Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kusoma vitabu

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Unakufa Taratibu… Bila Hata Kujua Sababu? HUJISOMEI!

  ‎‎Unajua nini kaka/dada…  Kuna maumivu huwa hayapigi kelele. ‎Hayaleti presha. Hayajulikani fasta. ‎Yanakuja polepole… kimyakimya… mpaka siku moja unajikuta umepotea kabisa. ‎ ‎Na moja ya maumivu hayo ni… ‎Maisha Bila Kusoma Vitabu. ‎ ‎Soma hapa sasa: ‎Watu wengi wanaishi kama vile kusoma ni kwa ajili ya shule tu. ‎Au ni kitu cha wasomi. ‎Au ni “luxury” ya watu wanaotafuta PhD. ‎ ‎Lakini ukweli ni huu: ‎Maisha Bila Kusoma ni kama gari bila mafuta. ‎Unalipenda. Unalipiga mswaki kila asubuhi. ‎Lakini halisogei. ‎Linasimama pale pale, siku baada ya siku. ‎ ‎Umeshajiuliza kwanini maisha yako yamekuwa magumu hivi? ‎Kwanini kila mwaka una malengo… lakini hakuna kinachobadilika? ‎ ‎Kwanini wengine wanakimbia… na wewe unatembea? ‎Au hata kutambaa ni kazi? ‎ ‎Ni kama dunia inasonga mbele… lakini wewe umesahaulika. ‎Unajituma. Unahangaika. ‎Lakini bado maisha hayakusikilizi. ‎ ‎Na wakati wewe unapiga miayo ukiangalia TikTok… ‎wengine wanasoma makala, vitabu, kozi, wanajifunza skills… ...

‎Siri Ya Kusoma Vitabu Vingi Bila Kuvisahau.....

  ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Unasoma kitabu leo... kesho umesahau kila kitu. ‎Ushaona hiyo kitu? Inachosha. Inakatisha tamaa. ‎Unajikuta unasoma tu, lakini hamna unachobeba. ‎ ‎Kama umewahi kujisikia hivyo… karibu kwenye club yetu. ‎ ‎Lakini leo nataka nikuambie kitu cha maana sana. ‎Siri ambayo wengi hawajui. ‎Siri ya kusoma vitabu vingi bila kuvisahau. ‎Na kuvitumia kukuinua maishani. ‎ ‎ ‎Unasoma, unasahau. Unasoma, unasahau. ‎Kama vile ubongo wako unazima mara tu ukifunga kitabu. ‎Unajikuta unarejea kwenye maisha ya zamani. ‎ ‎Unasema “Aaah, kile kitabu kilikuwa kizuri sana…” ‎Lakini ukuliza ulijifunza nini? Unashindwa kusema. ‎ ‎Inaumiza. Sana. ‎Ni kama unakula chakula kizuri, lakini mwili wako haukipokei. ‎Hakuna nguvu. Hakuna mabadiliko. Hakuna matokeo. ‎ ‎Lakini tatizo si wewe. ‎Tatizo ni mbinu unayotumia. ‎Watu wengi husoma vitabu kama vile wanasoma gazeti. ‎ ‎Wanakimbia. Wanamaliza haraka. ‎Wanataka kumaliza kurasa nyingi bila kutafuna kilichoandikwa. ‎ ‎Halafu wanashanga...

‎Faida 7 Za Kipekee Za Kusoma VITABU Kila Siku Hata Kama Ni DAKIKA 10 TU!

Picha
 ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Watu wengi wanalalamika hawafanikiwi. ‎ ‎Wanajitahidi sana lakini hakuna hatua zozote wanazopiga. ‎ ‎Wengine kila siku wako online lakini akili zao ziko offline. ‎ ‎Kila mtu anatafuta "shortcut ya mafanikio", lakini wanakosa kitu kimoja cha msingi... ‎ ‎Kusoma vitabu. ‎ ‎Ndiyo, hata kama ni dakika 10 tu kwa siku, inaweza kubadilisha kila kitu. ‎ ‎Hebu fikiria… ‎ ‎Miaka mitano ijayo, utakuwa mtu yule yule tu, isipokuwa tu kwa vitu viwili: ‎ ‎Vitabu ulivyosoma, na watu ulioambatana nao. ‎ ‎Sasa kama kila siku unasoma status, memes na story za watu… ‎ ‎Lakini huwezi kusoma hata ukurasa mmoja wa kitabu, unajidhulumu mwenyewe. ‎ ‎Mafanikio hayaji kwa kuomba omba—yanakuja kwa maarifa. ‎ ‎Na maarifa yapo vitabuni. ‎ ‎Ukikwepa kusoma leo, utajikuta unakumbana na matatizo yale yale kesho. ‎ ‎Kuna watu wanasema, “Mimi siwezi kusoma vitabu.” ‎ ‎“Nachoka haraka.” ‎ ‎"Usomaji sio vitu vyangu." ‎ ‎Wanajikosea sana. ‎ ‎Hakuna mtu yeyote aliyezaliwa akij...