Ukweli Wa Kushangaza: Mara Ya Pili Nilipokisoma… Ndipo Nilipokisoma Kwa Mara Ya Kwanza.....
Je, unapaswa kusoma kitabu mara moja au mara nyingi? Hadithi hii itakupa jibu la moyo.... Nilikuwa na orodha ndefu ya vitabu. Niliamini mafanikio yangu yanategemea idadi ya vitabu nilivyomaliza. Nikawa najisifu: “Nimesoma vitabu 12 mwaka huu!” Lakini cha kushangaza, sikumbuki hata sura ya kwanza ya vitabu vitano. Nilikuwa msomaji mwenye kasi, lakini si mwenye mabadiliko. Siku moja nikakutana na nukuu: Don’t just read more books. Reread the right ones. Nukuu hiyo ilinichoma kama sindano ya kweli. Nikajiuliza: “Ina maana nasoma sana lakini bado nipo palepale?” Nilijitetea: “Mbona kusoma kitabu mara moja tu inatosha? Sina muda wa kurudia! Kuna vitabu vingapi bado sijavifungua? Niliona kurudia kitabu kama kurudia darasa uliokwisha kufaulu. Lakini ndani kabisa, nilihisi kuna kitu kinakosekana. Nikamkuta mjasiriamali mmoja aliyenukuliwa kwenye podcast: .Mimi husoma vitabu vichache lakini kila mwaka narudia vitabu vitatu muhimu. ...