Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...
Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... Nilikuwa nimehitimu shule. Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” Sikupata kazi niliyoitegemea. Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. Siku moja nikakutana na nukuu: “Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain Nikaanza kujiuliza: "Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" Nikapuuzia. Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. Mbona havifundishwi shuleni? Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: "Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” Akaniongeza na kingine: “The 7 Habits of ...