Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...
Hii hapa safari ya kugusa moyo wako.
Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?....
Nilikuwa nimehitimu shule.
Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani.
Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.”
Sikupata kazi niliyoitegemea.
Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?"
Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha.
Siku moja nikakutana na nukuu:
“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain
Nikaanza kujiuliza:
"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?"
Nikapuuzia.
Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana.
Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa.
Mbona havifundishwi shuleni?
Mbona havijasheheni nadharia na mitihani?
Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia:
"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua."
Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.”
Akaniongeza na kingine:
“The 7 Habits of Highly Effective People.”
Nikaanza kusoma lakini si kama mwanafunzi wa shule, bali mwanafunzi wa maisha.
Siku moja, nilisoma mstari mmoja tu ambao ulibadilisha maisha yangu:
“Mtu maskini hufanya kazi kwa pesa, mtu tajiri hufanya pesa imfanyie kazi.”
Nikahisi kama akili yangu imeunganishwa tena kwa mara ya pili.
Nilianza kufungua macho ya maisha kwa mara ya kwanza kwa hiari yangu.
Wengine waliniona kama nimepotea:
Unaacha kusaka kazi na kusoma vitabu vya mabepari?
Lakini mimi niliendelea.
Nikaanza kuandika mafunzo.
Nikaanza kuchukua hatua ndogo.
Nilipokutana na changamoto za maisha, nilikuwa na silaha maarifa.
Nilipoanzisha biashara yangu ya kwanza, nikapata hasara.
Nilikuwa na kila sababu ya kukata tamaa.
Lakini nikakumbuka nilichosoma:
"Failure is part of learning. Keep moving."
Nikanyanyuka, nikasahihisha kosa, na safari ikaendelea.
Leo nimejifunza:
📌 Kusoma vitabu ni kama kuongea na wakubwa bila kuwa na miadi.
📌 Kila kitabu bora ni darasa jipya.
📌 Maisha hayana mitaala, bali yamejaa mitihani ya ghafla.
📌 Vitabu vina majibu ambayo shule haikuwahi kunipa.
Sasa naandika kila kitabu ninachosoma,
Ninafundisha wengine,
Na nimejenga tabia ya kuwa mwanafunzi kila siku sio kwa ajili ya daraja, bali kwa ajili ya maisha.
Mimi si mtu yule wa mwanzo.
Nimekuwa mwanafunzi wa maisha.
Kila siku ni somo.
Kila changamoto ni mtihani.
Na kila kitabu ni mwalimu mpya.
Rafiki, kama unaishi kama vile umeshahitimu kila kitu umeshaanza kushindwa.
Maisha huwatunuku wanafunzi wa kweli.
Soma. Tafakari. Tumia.
Usome kwa ajili ya mabadiliko, si kwa ajili ya kujisifu.
Kitabu kimoja kinaweza kuwa kozi ya maisha yako.
Piga simu au tuma meseji, Kwenda 0750376891.
Upate vitabu vya Kiingereza na Vya kiswahili Na Vilivyotafsiriwa Kwa Lugha Rahisi Kabisa.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali,
Kocha Ramadhan Amir
Mwandishi| Mkufunzi Wa Mauzo Ya MAFANIKIO | Kocha Wa Mafanikio Ya Mauzo|
Maoni
Chapisha Maoni