Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Jinsi ya Kuacha Kuomba Wateja na Kuanzisha Biashara Inayovutia Wateja Wenyewe Kwa Thamani

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Acha Kuomba Anza Kuitwa….

Picha
Rafiki Yangu, Miaka mitatu (3) iliyopita, Nilikutana na kijana mmoja ambaye aliniambia,  “Kaka, mimi huandika inbox 50 kwa siku hakuna anayejibu.  Wengine hata huniblock.” Nilimtazama kwa upole nikamwambia,  “Labda tatizo si watu ni wewe kuomba badala ya kuvutia.”  Siku hizi biashara si ya kuomba omba huruma, ni ya kujijenga kiasi kwamba watu wenyewe wanakuja kukuomba uwauzie.  Uliposikia kuhusu kampuni kama Apple, walikuita au uliwakimbilia?  Ndiyo maana leo tunasema: acha kuomba anza kuitwa. Somo hili utajifunza. Jinsi ya kuacha kuomba wateja bila mafanikio, Njia za kujijenga ili wateja wakutafute wenyewe, Mbinu za kuvutia badala ya kusumbua,Mitazamo mipya ya kibiashara inayokufanya uonekane wa thamani kubwa. Fikiria ukiamka asubuhi na unakuta ujumbe: "Habari, nimesikia kuhusu huduma yako, naomba unisaidie… "Watu wanaku-tag mitandaoni, wanakutumia referrals, wanakutafuta wenyewe.  Umeacha kusukuma watu sasa unavutia kwa nguvu.  Unapumua kwa raha...