Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kumbukumbu ya Kusoma Mbinu za Kusoma Jinsi ya Kumbuka Vitabu Elimu ya Vitabu Nguvu ya Kusoma Tips za Kujifunza Usomaji Bora Ramadhan Amir Mkufunzi Kumbukumbu ya Haraka Kusoma Bila Kusahau

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

Picha
  ‎ ‎Ukipitia hii, kumbukumbu zako zitakuwa kama za kasuku aliyefundishwa kuimba chorus ya Diamond... ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Unasoma kitabu leo… ‎ ‎Kesho haukumbuki hata ukurasa wa kwanza. ‎ ‎Ukiulizwa ulichojifunza, unazubaa kama umepigwa na butwaa. ‎ ‎Unajikuta unasoma tu ilimradi umalize, si kwa sababu unaelewa au utakumbuka. ‎ ‎Yani unatumia muda wako kusoma… ‎ ‎Unaweka akiba ya maneno kichwani… ‎ ‎Halafu akili inafuta kila kitu kama flash drive yenye virus! ‎ ‎Unasoma vitabu vingi, ila akili haina ushahidi wowote. ‎ ‎Inapoteza kumbukumbu kama ex wako aliyesahau yote mliyowahi kupitia. ‎ ‎Lakini mbona kuna wengine wakisoma, wanakumbuka hadi mistari ya mwisho? ‎ ‎Hii ndo pointi ya kukasirikia! ‎ ‎Sio kwamba Huna Akili. ‎ ‎Sio kwamba huna uwezo. ‎ ‎Ni mbinu tu unazotumia ndizo za kizamani. ‎ ‎Zile za kukariri bila kuelewa, au kusoma harakaharaka kama unakimbizana na deadline ya NECTA. ‎ ‎Zisahau. Hapa nakuletea...