Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya elimu ya kiuchumi

‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

Unapuuza Silaha Inayoweza Kukutoa Kwenye Umasikini, Kila Siku Bila Kujua!...

Picha
 ‎ ‎Rafiki Yangu Mpendwa, ‎ ‎Wewe unateseka. ‎Kila siku unakimbizana kutafuta hela. ‎Lakini maisha yako bado ni yaleyale. ‎Unajua kwanini? ‎ ‎Kwa sababu unapuuza silaha moja rahisi sana: KITABU. ‎ ‎Ndiyo, kile kitu unachokiona kama vya wasomi pekee. ‎Kile unachosema “Mimi si mtu wa kusoma.” ‎Hicho ndicho kinachokuweka hapo ulipo. ‎ ‎Vitabu ni Siri ya Mafanikio. ‎Zimebeba akili za matajiri, wabunifu, na watu waliokwishapitia ulichonacho. ‎Lakini wewe unapita navyo kama takataka. ‎ ‎Hebu jiulize... ‎Kila siku unatumia masaa 4 kwenye TikTok, Insta, na kuangalia video za utani. ‎Lakini dakika 15 kusoma kitabu? ‎Huipati! ‎ ‎Halafu unataka utajiri... ‎Unataka biashara izae... ‎Unataka maisha ya mamilionea... ‎Lakini hutaki kujenga ubongo wa kimamilionea! ‎ ‎Huwezi kuwa tajiri kwa akili ya kupenda starehe na uvivu wa maarifa. ‎Wewe ndiye unajizuia mwenyewe! ‎ ‎Wengi wanasema, “Aaah vitabu havisaidii.” ‎Huo ni uongo uliopakiwa kwa ujinga. ‎ ‎Vitabu vimewabadilisha watu: ‎Waliokuwa maskini ...