Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya vitabu vya pesa

‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

‎Hii Ndiyo Siri Elon Musk Aliyoificha: Vitabu 5 Vilivyompa Akili Ya Mabilioni!

Wengi tunapenda mafanikio ya Elon Musk. ‎Tunasikia Tesla, tunatamani SpaceX, tunatamani kuwa kama yeye. ‎ ‎Lakini hatujui alifika vipi hapo. ‎Wengi tunahangaika bila ramani. ‎Tunapoteza muda TikTok, tunazunguka kwenye magroup ya WhatsApp bila mwelekeo. ‎ ‎Elon hakujifunza mambo haya darasani. ‎Alijifunza vitabuni. ‎Ndiyo, vitabu. ‎ ‎Na si vitabu vya "Jinsi ya Kupata Mpenzi Kwa Siku Moja!" ‎Ni vitabu vya kuchonga akili kuwa mashine ya kutengeneza mabilioni. ‎ ‎Unalala na simu mkononi. ‎Unasubiri motivator wa Instagram akuvutie kwa clip ya sekunde 15. ‎ ‎Wewe bado unasema “Siku moja nitafanikiwa!” ‎Lakini Elon Musk alikula vitabu. ‎Aliwasoma kina Benjamin Franklin, kina Asimov. ‎ ‎Wewe unasoma tu captions za memes. ‎Na unategemea maisha yabadilike? ‎ ‎Utaendelea tu kufuta machozi kwenye pillow ya bei rahisi. ‎ ‎Watu wengi wanaamini mafanikio ni “Koneksheni” tu. ‎Ama eti ni lazima uzaliwe kwenye familia ya kitajiri. ‎ ‎Elon hakuzaliwa hivyo. ‎Alikua bullied, alikua mpweke, aliku...