Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya jinsi ya kusoma bila kusahau

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Siri Ya Kusoma Vitabu Vingi Bila Kuvisahau.....

  ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Unasoma kitabu leo... kesho umesahau kila kitu. ‎Ushaona hiyo kitu? Inachosha. Inakatisha tamaa. ‎Unajikuta unasoma tu, lakini hamna unachobeba. ‎ ‎Kama umewahi kujisikia hivyo… karibu kwenye club yetu. ‎ ‎Lakini leo nataka nikuambie kitu cha maana sana. ‎Siri ambayo wengi hawajui. ‎Siri ya kusoma vitabu vingi bila kuvisahau. ‎Na kuvitumia kukuinua maishani. ‎ ‎ ‎Unasoma, unasahau. Unasoma, unasahau. ‎Kama vile ubongo wako unazima mara tu ukifunga kitabu. ‎Unajikuta unarejea kwenye maisha ya zamani. ‎ ‎Unasema “Aaah, kile kitabu kilikuwa kizuri sana…” ‎Lakini ukuliza ulijifunza nini? Unashindwa kusema. ‎ ‎Inaumiza. Sana. ‎Ni kama unakula chakula kizuri, lakini mwili wako haukipokei. ‎Hakuna nguvu. Hakuna mabadiliko. Hakuna matokeo. ‎ ‎Lakini tatizo si wewe. ‎Tatizo ni mbinu unayotumia. ‎Watu wengi husoma vitabu kama vile wanasoma gazeti. ‎ ‎Wanakimbia. Wanamaliza haraka. ‎Wanataka kumaliza kurasa nyingi bila kutafuna kilichoandikwa. ‎ ‎Halafu wanashanga...