Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kusoma kila siku

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Soma Dakika 15 Kila Siku: Njia Rahisi Ya Kuvunja Umasikini Na Kujenga Utajiri...

 ‎Rafiki Yangu... ‎ ‎Unalala na simu mkononi. ‎Unamka na WhatsApp, Insta, na bet. ‎Hujawahi kukaa chini usome dakika 15 hata siku moja. ‎ ‎Na bado unajiuliza, “Mbona maisha hayaendi?” ‎Sasa sikia… ‎ ‎Watu wengi wanadhani utajiri unatokana na bahati. ‎Au kuwa na baba tajiri. ‎Au kufungua biashara kubwa ghafla. ‎ ‎Hawajui siri moja ya ajabu: ‎Dakika 15 tu za kusoma kila siku zinaweza kubadili kila kitu. ‎ ‎Sio lazima usome vitabu vigumu kama vya sayansi. ‎La hasha. ‎Unaweza kusoma kuhusu pesa, biashara, akili, au tabia za mafanikio. ‎ ‎Ni kama kuchoma mafuta polepole lakini mwisho gari linafika mbali sana. ‎ ‎Lakini unajua kinachoumiza zaidi? ‎Watu wanaosema “mimi sibadiliki kwa kusoma!” ‎Wanasema hivyo wakiwa broke. ‎Wakiwa wamechoka na maisha. ‎Wakilia usiku, wakicheka mchana. ‎ ‎Wanataka pesa, heshima, uhuru… ‎Lakini hawako tayari kusoma hata ukurasa mmoja kwa siku. ‎ ‎Wanakataa kusoma lakini wanakubali kuumia. ‎Wanachoka kusubiri neema ya ghafla, wakati wenyewe wamekata neema ya ...