Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Copywriting vs Content Copywriting ni nini Content ni nini Uandishi unaouza Mauzo kwa maneno Copy kwa biashara Tofauti za uandishi Maneno ya kuuza Uandishi wa matangazo

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

Hii Ndiyo Tofauti Ya COPYWRITING Na Content WRITING Wanaokuficha! 💥

‎ ‎Unajua nini? ‎Watu wengi wanajifanya waandishi, ‎Lakini wanachanganya Copywriting na Content Writing kama maji na mafuta! ‎ ‎Ni kama kuchanganya kuchoma chipsi na kufua nguo… ‎Vyote ni kazi, lakini si sawa hata kidogo! ‎ ‎Leo nakufungua macho. ‎Utaelewa tofauti kubwa sana kati ya Copywriting na Content Writing. ‎Ukimaliza kusoma hii makala, utajua ni ipi inalipa, ipi ni sanaa ya kuuza, ‎na ipi inaweza kukutoa kapa kama huitumii vizuri. ‎ ‎Fikiria upo na laptop yako, ‎Unaandika sentensi chache tu… ‎Baada ya dakika chache, mtu anakutumia pesa. ‎ ‎Copy zako zinauza bidhaa. ‎Waandishi wakubwa wa Copywriting wanalipwa hadi MILIONI kwa barua moja tu! ‎Wanaandika post moja, inauza bidhaa elfu moja. ‎ ‎Sasa waza tena… ‎Unatumia muda mwingi kuandika content, ‎Una likes, una comments, lakini hakuna mtu anayebonyeza "nunua sasa". ‎Ni kama kupiga kelele kwenye jangwa. ‎ ‎Hebu muangalie Joseph Sugarman, mmoja wa magwiji wa Copywriting. ‎Alikuwa akiandika matangazo ya kurasa 2, ‎na watu...