Jinsi Kusoma Vitabu Kunavyobadilisha Ubongo Wako....
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Rafiki Yangu,
Miaka michache iliyopita, nilikuwa mtu wa kawaida sana.
Nilikuwa na ndoto kubwa… lakini akili iliyochoka.
Kichwa kilijaa mazungumzo ya watu, si ndoto zangu.
Nilikuwa nikiamka asubuhi nikijiuliza, “Hivi akili yangu inafanya kazi kwa asilimia ngapi tu?”
Sikujua kuwa kitu kimoja kidogo kingeweza kubadilisha kabisa maisha yangu.
Siku moja, nikiwa napitia changamoto za maisha, nilikutana na kitabu kidogo cha kurasa 120.
Jina lake lilikuwa ni "Change Your Thinking Change Your Life”
Kwa dharau nikasema, “Kitabu gani hiki? Kitatofautisha nini?”
Lakini kuna sauti ndani yangu ilisema:
“Jaribu. Una nini cha kupoteza?”
Nilikubali… Nikaanza kusoma.
Mwanzo kilikuwa kigumu. Ubongo wangu ulitaka kuachana nacho.
Nilikuwa nimezoea starehe, sio maarifa.
Nilikuwa mwepesi wa kuangalia video, sio kusoma kurasa.
Lakini kwa namna ya ajabu kila ukurasa niliomaliza, akili yangu iliongezeka nguvu.
Nilianza kuona vitu nilivyokuwa sivioni.
Nilianza kufikiri kwa undani, kuelewa kwa haraka, na kuhoji kwa busara.
Baada ya vitabu 10, nilikuwa tofauti kabisa.
Nilielewa jinsi ubongo wangu unavyofanya kazi.
Nilijua kwa nini nilikuwa nikichelewa kufanya maamuzi.
Nilijua kwa nini nilikuwa nikiahirisha mambo muhimu.
Vitabu ni kama “chakula cha akili” kila ukurasa ulijenga misuli ya kufikiri.
Uwezo wangu wa kuelewa, kupambanua mambo, na kutatua matatizo uliongezeka mara mbili… mara tatu!
Leo hii, mimi ndiye watu wanamgeukia kushauriwa.
Mimi ndiye ninaleta suluhisho mezani.
Mimi ndiye ninayeandika, ninayeongoza, ninayefikiri kwa kina.
Na nilichogundua ni hiki:
👉 “Ubongo wako ni kama misuli. Ukiusomesha, unakuwa shujaa.”
👉 “Kitabu ni kama kocha wa ndani. Kinazungumza na akili yako kimya kimya lakini kwa sauti yenye nguvu isiyofutika.”
Kama unahisi una uwezo mkubwa lakini haueleweki…
Kama kila siku unahisi unajichanganya, unakosa dira, au unafanya maamuzi mabaya…
Basi usisubiri hadi maisha yakufundishe kwa maumivu.
🧠 Anza leo.
Chukua kitabu.
Soma kila siku hata kurasa mbili.
Ubongo wako utakushukuru kwa miaka kumi ijayo.
💡 Kwa sababu: “Tofauti kati ya kichwa kinachojua na kisichojua…
ni kurasa chache tu zilizosomewa kwa makini.”
📘 Safari ya ubongo wako inaanza kwa kitabu kimoja tu.
Je, uko tayari kuwa shujaa wa akili yako?
Anyway, Kama Unataka Kupata Vitabu Vizuri, Piga Simu 0750376891,
Karibu.
Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni