Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Vitabu

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Ni Jinsi Gani Naweza Kuendeleza Tabia Ya Kusoma Kila Siku?

 ‎ 🛤️ Hadithi ya Safari Yangu Ya Kusoma: ‎ ‎ Kutoka Kutojali Mpaka Kutegemea Kitabu Kama Maji ‎ ‎Miaka 15 iliyopita, mimi ndiye ningeweza kutoa sababu zote kwanini "kusoma si muhimu sana." ‎ ‎Nilikuwa na ratiba ngumu. Kila siku nikikurupuka asubuhi, nikiingia kwenye harakati za maisha bila kusoma hata ukurasa mmoja. ‎ ‎Nilikuwa na vitabu kabatini lakini vilikuwa kama mapambo. Vilikuwepo kwa heshima, si kwa matumizi. ‎ ‎Nilijifariji kwa kusema: “Mimi ni mtu wa vitendo, si maneno.” ‎Lakini ndani kabisa, nilijua kuna kitu napoteza. ‎ ‎Siku moja, nikiwa kwenye Facebook, nikamuona kijana mmoja akisema: ‎ ‎“Kama huwezi kujenga tabia ya kusoma kila siku, usitarajie kujenga biashara inayodumu, akili inayotulia, au maisha yenye dira.” ‎ ‎Mistari hiyo ilinipiga kama radi. ‎Niliisikia kweli ndani yangu. Nikagundua: ndiyo sababu najichanganya, najisahau, najiumiza ni kwa sababu najikosa. ‎ ‎Ndipo nilipoamua: Lazima niwe mtu wa kusoma kila siku. ‎ ‎Mabadiliko hayaji kirahisi. Nilijaribu ...

‎ ‎Kwa Nini Watu Maskini Hawapendi Kusoma Vitabu

Picha
 ‎ ‎Kaka/Dada, Huu Ni Ukweli Unaoumiza Lakini Utakusaidia. ‎ ‎Maskini wengi hawapendi kusoma vitabu. ‎ ‎Umeshawahi kujiuliza kwa nini? ‎ ‎Yaani mtu anaishi maisha magumu… ‎ ‎Lakini ukimpatia kitabu cha bure chenye maarifa ya kutoka hapo alipo anakudharau. ‎ ‎Akiwa online, anaweza kucheka video 20 za utani… ‎ ‎Lakini video moja tu ya mafanikio, ya dakika mbili ataisema: ‎ ‎“Hayo mambo ya matajiri.” ‎ ‎Hapo ndipo utagundua: ‎ ‎Umaskini hauanzi mfukoni… unaanzia kichwani. ‎ ‎Tatizo Halipo Tu Kwenye Pesa ‎ ‎Watu wengi waliokata tamaa si kwamba hawana pesa... ‎ ‎Ni kwamba hawana maarifa. ‎ ‎Wanajua mpira, wanajua drama za mastaa, wanajua nani kapigana na nani... ‎ ‎Lakini hawajui jinsi ya kuongea vizuri ili wapewe kazi. ‎ ‎Hawajui njia rahisi ya kuweka akiba kidogo kila wiki. ‎ ‎Hawajui hata kusoma CV yao vizuri. ‎ ‎Sababu? ‎ ‎Hawajawahi kupewa nafasi ya kuamini kuwa vitabu vinaweza kuwasaidia. ‎ ‎Kuna Uongo Umekaa Kama Ukweli ‎ ‎ “Mimi si mtu wa vitabu.” ‎ ‎ “Mimi shule ilinichosha.” ‎...