Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya maendeleo

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Ni Jinsi Gani Naweza Kuendeleza Tabia Ya Kusoma Kila Siku?

 ‎ 🛤️ Hadithi ya Safari Yangu Ya Kusoma: ‎ ‎ Kutoka Kutojali Mpaka Kutegemea Kitabu Kama Maji ‎ ‎Miaka 15 iliyopita, mimi ndiye ningeweza kutoa sababu zote kwanini "kusoma si muhimu sana." ‎ ‎Nilikuwa na ratiba ngumu. Kila siku nikikurupuka asubuhi, nikiingia kwenye harakati za maisha bila kusoma hata ukurasa mmoja. ‎ ‎Nilikuwa na vitabu kabatini lakini vilikuwa kama mapambo. Vilikuwepo kwa heshima, si kwa matumizi. ‎ ‎Nilijifariji kwa kusema: “Mimi ni mtu wa vitendo, si maneno.” ‎Lakini ndani kabisa, nilijua kuna kitu napoteza. ‎ ‎Siku moja, nikiwa kwenye Facebook, nikamuona kijana mmoja akisema: ‎ ‎“Kama huwezi kujenga tabia ya kusoma kila siku, usitarajie kujenga biashara inayodumu, akili inayotulia, au maisha yenye dira.” ‎ ‎Mistari hiyo ilinipiga kama radi. ‎Niliisikia kweli ndani yangu. Nikagundua: ndiyo sababu najichanganya, najisahau, najiumiza ni kwa sababu najikosa. ‎ ‎Ndipo nilipoamua: Lazima niwe mtu wa kusoma kila siku. ‎ ‎Mabadiliko hayaji kirahisi. Nilijaribu ...