Nilikuwa Naogopa Kila Kitu… Mpaka Niliposoma Kitabu Kimoja Tu...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Miaka ya nyuma,
Mariam alikuwa binti mwenye ndoto kubwa, lakini mwenye sauti ndogo sana mbele ya watu.
Kila alipokuwa na wazo, moyo wake ulitetemeka kusema.
Kila alipohitaji kuongea mbele ya kundi, hata marafiki tu, alinyamaza.
Alikuwa anajilaumu kimya kimya:
“Mbona naona kila mtu ana ujasiri isipokuwa mimi?”
Siku moja, alihudhuria kikao cha wanawake wajasiriamali.
Mwanamke mmoja akasimama na kuongea kwa ujasiri wa kuvutia.
Baada ya mkutano, Mariam akamwendea kwa woga na kumuuliza:
"Ulikuwa na ujasiri mkubwa! Siri yako ni nini?"
Akamjibu kwa tabasamu:
“Nilianza kusoma vitabu. Si vitabu vya shule, bali vya maisha.”
Mariam alitabasamu tu na kusema kwa sauti ya chini:
"Mimi siwezi kuwa msomaji. Nikiwaza tu kurasa kumi, nashikwa na usingizi."
Lakini moyo wake haukutulia.
Usiku ule alitafakari:
"Kama kusoma vitabu kunabadilisha watu labda na mimi nitaweza."
Siku iliyofuata, alitumiwa link ya kujiunga na group la WhatsApp.
Ilisomeka:
“Jifunze kila siku jinsi ya kuongeza kujiamini kupitia usomaji. Mafunzo haya ni bure kabisa. Wasiliana: 0750376891.”
Alijiunga.
Somo la kwanza lilimliza:
“Huwezi kuongea kwa ujasiri nje, kama huongei na nafsi yako ndani kwa maarifa.”
Mariam aliahidi: “Nitamaliza kitabu kimoja. Tu kimoja.”
Alichukua kitabu kilichopendekezwa ndani ya group.
Kila ukurasa alioumaliza, alihisi akijijenga.
Kila sentensi ilimfanya ajiangalie upya.
Alianza kuandika pointi ndogo na kuziweka kwenye kioo chake.
Wengine kwenye group walimpa moyo.
Walipeana changamoto: “Sema kitu kimoja mbele ya watu wiki hii.”
Mariam akakubali.
Alipoanza kuzungumza, alihisi ulimi wake ukitetemeka lakini maneno yakatoka.
Watu walishangilia.
Kwa mara ya kwanza, alihisi:
“Nina thamani. Nina sauti.”
Muda si mrefu, Mariam aliitwa kutoa maoni kwenye hafla ya mtaa wao.
Alitetemeka, lakini akakumbuka somo la siku ya saba kutoka kwenye group:
“Ujasiri si kukosa hofu ni kufanya jambo licha ya hofu hiyo kuwepo.”
Aliinuka.
Akaongea kwa dakika mbili.
Ukumbi ukatulia.
Watu wakapiga makofi.
Moyo wake ukalia kwa furaha.
Leo hii, Mariam ni mhamasishaji wa wasichana wadogo.
Anawafundisha kusoma vitabu, kujieleza, na kujiamini.
Anasema:
“Sikuwahi kufikiri maneno kwenye kurasa yangebadilisha maisha yangu lakini yamefanya hivyo.”
Mariam hushiriki namba hii kwa kila mtu mwenye ndoto ya kujiamini zaidi:
📞 0750376891
Anawaambia kwa sauti ya upendo:
“Jiunge na group hili. Jifunze kidogo kila siku.
Utajijua, utajikubali, na dunia itakuamini.”
Soma kidogo. Jifunze kidogo. Badilika sana.
👉 Jiunge leo kwenye Group la WhatsApp la mafunzo ya bure.
📞 0750376891
Usisahau kuwashirikisha wengine wapo waliokata tamaa ya maisha kwa sababu hawajui nguvu ya kurasa chache tu.
👉 Waalike. Wape zawadi ya mabadiliko.
Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Ramadhani Amir,
Mwandishi| Mkufunzi Wa Mauzo Yenye MAFANIKIO| Kocha Wa Mafanikio Ya Mauzo
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni