Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Dawa ya kupenda kusoma vitabu: Mbinu ya ukurasa wa asubuhi inayokufanya ufurahie kusoma kila siku

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Huwa Hupendi Kusoma Vitabu? Hii Ndiyo Dawa Yako*….

 Rafiki, Hupendi Kusoma? Subiri Uone Siri Hii. Rafiki Yangu, Ulishawahi kushika kitabu, na ukasoma kurasa mbili tu, ukachoka hoi bin taabani? Kurasa mbili tu zikaonekana kama umebeba mawe ya Mtwara? Kuna watu hawapendi kabisa kusoma. Si kwa sababu hawana akili, wala hawajui kusoma, la! Ni kwa sababu ubongo wao umezoea burudani rahisi kama TikTok, Instagram, video za dakika moja mpaka kitabu kinaonekana kama maumivu. Na kumbuka, hatukuzaliwa tukiwa hatupendi kusoma. Hiyo chuki ya vitabu ni tabia iliyojengeka kidogo kidogo.  Ulipoanza shule labda ulikuwa na shauku, lakini ulipoambiwa usome vitabu visivyo na ladha, bila mtu kukuonyesha maana yake kwenye maisha yako, ukaanza kuviona kama adui. Halafu ukakua, ukaingia kwenye maisha ya kila siku, kazi, msongo, bili na sasa hata kurasa tano zinaonekana kama mzigo. Lakini ukweli mchungu ni huu: Kama huwezi kufurahia kusoma, unajinyima njia rahisi zaidi ya kujua siri za maisha. Nikupe stori ya Baba Rashid, dereva wa bodaboda pale Sinza...