Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maendeleo Binafsi

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Nilikuwa Naogopa Kila Kitu… Mpaka Niliposoma Kitabu Kimoja Tu...

 Miaka ya nyuma, Mariam alikuwa binti mwenye ndoto kubwa, lakini mwenye sauti ndogo sana mbele ya watu. ‎ ‎Kila alipokuwa na wazo, moyo wake ulitetemeka kusema. ‎ ‎Kila alipohitaji kuongea mbele ya kundi, hata marafiki tu, alinyamaza. ‎ ‎Alikuwa anajilaumu kimya kimya: ‎“Mbona naona kila mtu ana ujasiri isipokuwa mimi?” ‎ ‎Siku moja, alihudhuria kikao cha wanawake wajasiriamali. ‎ ‎Mwanamke mmoja akasimama na kuongea kwa ujasiri wa kuvutia. ‎ ‎Baada ya mkutano, Mariam akamwendea kwa woga na kumuuliza: ‎ ‎"Ulikuwa na ujasiri mkubwa! Siri yako ni nini?" ‎ ‎Akamjibu kwa tabasamu: ‎“Nilianza kusoma vitabu. Si vitabu vya shule, bali vya maisha.” ‎ ‎Mariam alitabasamu tu na kusema kwa sauti ya chini: ‎"Mimi siwezi kuwa msomaji. Nikiwaza tu kurasa kumi, nashikwa na usingizi." ‎ ‎Lakini moyo wake haukutulia. ‎Usiku ule alitafakari: ‎"Kama kusoma vitabu kunabadilisha watu labda na mimi nitaweza." ‎ ‎Siku iliyofuata, alitumiwa link ya kujiunga na group la WhatsApp. ...

‎Hii Ndiyo Siri Elon Musk Aliyoificha: Vitabu 5 Vilivyompa Akili Ya Mabilioni!

Wengi tunapenda mafanikio ya Elon Musk. ‎Tunasikia Tesla, tunatamani SpaceX, tunatamani kuwa kama yeye. ‎ ‎Lakini hatujui alifika vipi hapo. ‎Wengi tunahangaika bila ramani. ‎Tunapoteza muda TikTok, tunazunguka kwenye magroup ya WhatsApp bila mwelekeo. ‎ ‎Elon hakujifunza mambo haya darasani. ‎Alijifunza vitabuni. ‎Ndiyo, vitabu. ‎ ‎Na si vitabu vya "Jinsi ya Kupata Mpenzi Kwa Siku Moja!" ‎Ni vitabu vya kuchonga akili kuwa mashine ya kutengeneza mabilioni. ‎ ‎Unalala na simu mkononi. ‎Unasubiri motivator wa Instagram akuvutie kwa clip ya sekunde 15. ‎ ‎Wewe bado unasema “Siku moja nitafanikiwa!” ‎Lakini Elon Musk alikula vitabu. ‎Aliwasoma kina Benjamin Franklin, kina Asimov. ‎ ‎Wewe unasoma tu captions za memes. ‎Na unategemea maisha yabadilike? ‎ ‎Utaendelea tu kufuta machozi kwenye pillow ya bei rahisi. ‎ ‎Watu wengi wanaamini mafanikio ni “Koneksheni” tu. ‎Ama eti ni lazima uzaliwe kwenye familia ya kitajiri. ‎ ‎Elon hakuzaliwa hivyo. ‎Alikua bullied, alikua mpweke, aliku...

Utajiri Unaanza Na Dakika 15 Tu Kila Siku Na Hakuna Atakayekuanbia HILI!

‎‎Aliwahi kuwa maskini sana. Hakuwahi kumaliza hata kitabu kimoja maishani mwake. ‎ ‎Lakini siku moja, alijilazimisha kusoma dakika 15 tu kabla ya kulala. ‎Mwaka mmoja baadaye, alikuwa na biashara tatu, kipato cha kila siku, na uhuru aliokuwa akiuota. ‎ ‎Ni ajabu eeh? ‎Ndiyo. ‎Lakini si uchawi. Ni nguvu ya maarifa madogo kila siku. ‎ ‎Katika makala hii, nitakuonyesha jinsi dakika 15 tu za kusoma kila siku zinavyoweza kukutoa kwenye maisha ya kukopa hadi maisha ya kutajirika. ‎Nitakufundisha: ‎ ‎Nini cha kusoma ‎ ‎Jinsi ya kuanza ‎ ‎Na kwanini dakika 15 ni zaidi ya kutosha. ‎ ‎Fikiria maisha yako baada ya miezi 6: ‎Unaongea kwa ujasiri. ‎Unajua wapi pa kuwekeza. ‎Una wazo la biashara. ‎Unajua kutunza fedha zako. ‎Unajiamini zaidi. ‎Watu wanaanza kukuona tofauti. ‎Kila siku unakaribia mafanikio. ‎Na yote yalianza na kurasa chache tu kila jioni. ‎ ‎ ‎Watu maarufu kama Warren Buffett, Elon Musk, na Oprah Winfrey wamesema wazi “kusoma kila siku ndicho kilichowatengeneza.” ‎ ‎Buffett husoma ...

‎ ‎Kwa Nini Watu Maskini Hawapendi Kusoma Vitabu

Picha
 ‎ ‎Kaka/Dada, Huu Ni Ukweli Unaoumiza Lakini Utakusaidia. ‎ ‎Maskini wengi hawapendi kusoma vitabu. ‎ ‎Umeshawahi kujiuliza kwa nini? ‎ ‎Yaani mtu anaishi maisha magumu… ‎ ‎Lakini ukimpatia kitabu cha bure chenye maarifa ya kutoka hapo alipo anakudharau. ‎ ‎Akiwa online, anaweza kucheka video 20 za utani… ‎ ‎Lakini video moja tu ya mafanikio, ya dakika mbili ataisema: ‎ ‎“Hayo mambo ya matajiri.” ‎ ‎Hapo ndipo utagundua: ‎ ‎Umaskini hauanzi mfukoni… unaanzia kichwani. ‎ ‎Tatizo Halipo Tu Kwenye Pesa ‎ ‎Watu wengi waliokata tamaa si kwamba hawana pesa... ‎ ‎Ni kwamba hawana maarifa. ‎ ‎Wanajua mpira, wanajua drama za mastaa, wanajua nani kapigana na nani... ‎ ‎Lakini hawajui jinsi ya kuongea vizuri ili wapewe kazi. ‎ ‎Hawajui njia rahisi ya kuweka akiba kidogo kila wiki. ‎ ‎Hawajui hata kusoma CV yao vizuri. ‎ ‎Sababu? ‎ ‎Hawajawahi kupewa nafasi ya kuamini kuwa vitabu vinaweza kuwasaidia. ‎ ‎Kuna Uongo Umekaa Kama Ukweli ‎ ‎ “Mimi si mtu wa vitabu.” ‎ ‎ “Mimi shule ilinichosha.” ‎...