Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kwanini ni vigumu kusoma

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Kwa Nini Unaacha Kusoma Kitabu Kwenye Ukurasa wa 17? Hii Ndio Sababu Halisi (Na Inashangaza!)

Kwa Nini Ni Vigumu Kusoma Vitabu Mpaka Mwisho? ‎ ‎Kuna jamaa mmoja... ‎Anaitwa Musa Mfalme. ‎ ‎Sio mfalme kweli, lakini akili zake zilikuwa na hazina ya kifalme. ‎Alikuwa na ndoto kubwa sana. ‎Alitaka kuwa tajiri. ‎Mwenye maarifa. ‎Awe mtu wa tofauti. ‎ ‎Siku moja akapata kitabu. ‎Kikubwa. ‎Kimeandikwa kwa rangi ya dhahabu. ‎Juu yake kimeandikwa, ‎“Nguvu Ya Maarifa: Jinsi Ya Kujenga Maisha Yako Kuanzia Sasa.” ‎ ‎Akasema, ‎"Hili ndilo lililokuwa linanikimbia. Leo naanza, mpaka mwisho!" ‎ ‎Akasoma ukurasa wa kwanza. ‎Ukurasa wa pili. ‎Wa tatu... ‎Kichwa kinamwambia, “Bora uangalie TikTok kidogo tu…” ‎ ‎Akachukua simu. ‎Dakika mbili. ‎Zikawa saa moja. ‎Akasema, ‎"Kesho nitaendelea kusoma." ‎ ‎Hakurudi tena kwenye kile kitabu. ‎Mpaka leo. ‎ ‎Lakini Kwa Nini? Kwa Nini Tunashindwa Kumaliza Vitabu? ‎ ‎Hii hapa safari ya ukweli... ‎Safari ambayo Musa Mfalme alipitia na labda na wewe pia. ‎ ‎1. Vitabu Vinataka Nguvu Ya Ndani ‎ ‎Kusoma si kama kuangalia movie. ‎Hakuna kelele....