Kwa Nini Unaacha Kusoma Kitabu Kwenye Ukurasa wa 17? Hii Ndio Sababu Halisi (Na Inashangaza!)
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kwa Nini Ni Vigumu Kusoma Vitabu Mpaka Mwisho?
Kuna jamaa mmoja...
Anaitwa Musa Mfalme.
Sio mfalme kweli, lakini akili zake zilikuwa na hazina ya kifalme.
Alikuwa na ndoto kubwa sana.
Alitaka kuwa tajiri.
Mwenye maarifa.
Awe mtu wa tofauti.
Siku moja akapata kitabu.
Kikubwa.
Kimeandikwa kwa rangi ya dhahabu.
Juu yake kimeandikwa,
“Nguvu Ya Maarifa: Jinsi Ya Kujenga Maisha Yako Kuanzia Sasa.”
Akasema,
"Hili ndilo lililokuwa linanikimbia. Leo naanza, mpaka mwisho!"
Akasoma ukurasa wa kwanza.
Ukurasa wa pili.
Wa tatu...
Kichwa kinamwambia, “Bora uangalie TikTok kidogo tu…”
Akachukua simu.
Dakika mbili.
Zikawa saa moja.
Akasema,
"Kesho nitaendelea kusoma."
Hakurudi tena kwenye kile kitabu.
Mpaka leo.
Lakini Kwa Nini? Kwa Nini Tunashindwa Kumaliza Vitabu?
Hii hapa safari ya ukweli...
Safari ambayo Musa Mfalme alipitia na labda na wewe pia.
1. Vitabu Vinataka Nguvu Ya Ndani
Kusoma si kama kuangalia movie.
Hakuna kelele. Hakuna mwanga.
Ni wewe na kurasa.
Na mara nyingi, akili yako inasema:
"Hii kazi ni nzito. Hebu tupumzike kidogo."
2. Dunia Inapiga Kelele Sana
Simu inaita.
Meseji zinagonga.
Meme zimejaa.
Unapokaa kusoma, unashindana na kelele za dunia.
Unashindwa.
3. Hakuna Muundo Wako
Unakaa tu.
Bila ratiba.
Bila mfumo.
Bila hata lengo.
Kusoma bila direction ni kama kuendesha gari bila destination.
4. Unataka Haraka Sana
Unataka usome leo, ufanikiwe kesho.
Ukikuta ukurasa wa kwanza hauna “motisha,” unachoka.
Hujui kuwa maarifa yanachimbwa taratibu kama dhahabu.
5. Ulikosea Kitabu
Unasoma kile ambacho hakikuhusu.
Kitabu cha “Accounting for Engineers”
Na wewe hata calculator huna.
Lakini Musa Mfalme Alibadilika...
Siku moja alipokutana na mimi.
Nikamwambia,
"Soma kurasa mbili tu kila siku. Si zaidi. Si chini. Ila kila siku."
Musa akaanza.
Siku ya kwanza: kurasa mbili.
Siku ya pili: mbili.
Wiki moja: anasoma tano kwa siku.
Mwezi mmoja: amemaliza kitabu chake cha kwanza.
Hiyo ilibadilisha kila kitu.
Somo la Leo: Si Lazima Usome Saa Mbili… Anza Na Dakika Kumi Tu.
Hakikisha una ratiba.
Chagua vitabu vinavyogusa maisha yako.
Zima usumbufu wote kabla ya kusoma.
Na kumbuka: Ukianza na kurasa mbili kila siku, ndani ya mwaka utakuwa na kichwa kama cha Profesa.
Kama uliwahi kuanza kusoma kitabu ukakishia ukurasa wa 17...
Uko peke yako?
Hapana.
Karibu kwenye kundi la Musa Mfalme.
Lakini sasa, unaweza kutoka humo.
Anza leo. Kurasa mbili tu.
Usijidanganye tena.
Vitabu ni silaha. Ukizitumia, unashinda vita ya maisha.
Je, Wewe Ni Kama Musa Mfalme?
Niandikie kwenye comment.
Ama share hii makala na rafiki ambaye kila mara anasema:
"Mwaka huu nasoma vitabu kumi!"
Halafu hata kimoja hajamaliza.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.
0750376891.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni