Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Hadithi ya kweli ya kushinda msongo wa mawazo kupitia kusoma vitabu vya maarifa.

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Je, Vitabu Vinaweza Kuondoa Msongo wa Mawazo?....

 ‎Rafiki Yangu, ‎Bado namkumbuka.... ‎ ‎Alikuwa Hana Kitu. Sio Hela. Sio Mtaji. Sio Tumaini. ‎Jina lake ni Salma. Msichana wa kawaida kabisa kutoka familia ya kipato cha chini maeneo ya Mbagala.  ‎ ‎Baada ya kumaliza chuo kwa tabu, alipambana kutafuta kazi kwa miaka miwili bila mafanikio.  ‎ ‎Polepole, akaanza kupoteza matumaini. ‎Kila siku aliamka akiwa na hofu, akilala na mawazo. Alianza kujitenga na watu, hakupokea simu, na hata chakula kilimchosha.  ‎ ‎Msongo wa mawazo ukaanza kula akili yake taratibu. ‎ ‎Kila Kitu Kilibadilika Siku Aliyoangukia kwenye Kitabu. ‎Siku moja akiwa kwenye daladala, alimsikia mama mmoja akimsimulia rafiki yake kuhusu kitabu kinachoitwa Nguvu Ya Vitabu.  ‎ ‎Salma alijikuta akipata hamu ya kukisoma. Ingawa hakuwa na pesa, aliamua kuuza hereni zake ili kukinunua. ‎ ‎Kurasa za kwanza tu, zilianza kumbembeleza polepole kutoka kwenye giza la mawazo.  ‎ ‎Alianza kujifunza jinsi akili ya binadamu inavyoweza kubadilika kupitia maarifa...