Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Pesa Umasikini Mafanikio Elimu ya fedha Biashara Ramadhan Amir Hadithi ya kweli Motisha

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Kwa Nini Watu Wanakosa Pesa Ingawa Wanajituma?

‎Kakaa/Dadaa… ‎ ‎Umeshawahi kulala ukiwa umechoka sana, ‎ ‎Lakini bado huna hata shilingi mfukoni? ‎ ‎Umeamka mapema, ‎ ‎Ukapambana jua hadi linazama, ‎ ‎Ukavumilia kelele za mabosi, ‎Ukavumilia njaa kwa matumaini. ‎ ‎Lakini mwisho wa mwezi, ‎unahesabu senti. ‎ ‎Unaambiwa: *Jitume zaidi.* ‎Lakini unaumia moyoni, ‎kwa sababu umeshajituma mpaka unaungua ndani. ‎ ‎Kama hii ni hali yako, ‎najua uchungu unaoupitia. ‎ ‎Ni kama mbio zisizo na mwisho. ‎ ‎Unakimbia, lakini huoni mbele. ‎ ‎Unapiga hatua, lakini ni kama umerudi nyuma. ‎ ‎Wengine wanakucheka. ‎Wanasema huna akili ya pesa. ‎Lakini hawajui mateso yako. ‎ ‎Sasa sikiliza kwa makini... ‎ ‎Kazi ngumu pekee haitoshi. ‎Inauma kusema, lakini ni kweli. ‎ ‎Watu wengi wanaishia kuishi maisha ya mateso, ‎si kwa sababu hawajitumi, ‎bali kwa sababu hawajui cha kufanya na wanachopata. ‎ ‎Wanatumia kila walichonacho. ‎Hakuna mpango. ‎Hakuna akiba. ‎Hakuna uwekezaji. ‎Hakuna ndoto inayoelekea kutimia. ‎ ‎Na hapo ndipo ndoto nyingi hufia. ‎Ndipo ndo...