Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kujiamini

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Mtoto Wa Mchuuzi Aliyejijengea Ujasiri Kwa Kurasa...

 ‎Kijiji cha Msaranga kilijulikana kwa soko lake dogo lenye kelele nyingi na vumbi la kila asubuhi.  ‎ ‎Hapo ndipo alipokulia Amani, kijana mdogo, mtoto wa mchuuzi wa viazi. ‎ ‎Maisha yalikuwa magumu.  ‎ ‎Kila siku ilianza kwa sauti ya mama yake akimwamsha mapema: ‎ ‎“Amani, chukua ndoo, twende sokoni.” ‎ ‎Amani alikuwa mpole, mwenye aibu na asiyejiamini.  ‎ ‎Kila alipokuwa karibu na watu wengi, sauti yake ilikuwa ndogo kama ya kupiga dua moyoni.  ‎ ‎Alipoitwa darasani ajibu swali, alitetemeka. Watu walimcheka. Alijiona dhaifu. Akijisemea moyoni, ‎ ‎"Mimi siwezi kuwa kama wale watoto wanaoongea mbele za watu. Mimi si kitu." ‎ ‎Siku moja, akiwa anafagia meza sokoni, aliona karatasi la gazeti limefungiwa samaki.  ‎ ‎Katika lile karatasi, kulikuwa na maneno yaliomvutia: ‎ ‎ “Vitabu vinawafanya watu kuwa huru.” ‎ ‎Alishangaa. Akajiuliza, “Inawezekanaje kurasa tu zabadili maisha ya mtu?”  ‎ ‎Hapo ndipo moyo wake mdogo ukapata hamu ya kujua zaidi. ‎ ‎Lakini ...