Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kuvutia wateja

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Sanaa Ya Kuandika Kichwa Cha Habari Cha Kutosha Kuusimamisha MOYO Wa MTEJA

‎“Ukishika hii, unaweza kuuza barafu jangwa la Sahara” ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu.... ‎Unajua shida kubwa ya waandishi wengi wa matangazo? ‎Wanahangaika kuandika miandiko mizuri sana… ‎ ‎Lakini "kichwa cha habari chao ni cha kawaida sana". ‎ ‎Halafu wanashangaa kwa nini hakuna anaye-click. ‎ ‎Wanasema watu hawasomi. ‎Hapana. ‎ ‎Watu wanasoma ‎Wanasoma vichwa vya habari tu. ‎ ‎Kama kichwa hakishiki moyo… ‎Kama hakimshtui mteja… ‎Kama hakimfanyi asimame hata kama alikuwa anaenda chooni… ‎ ‎Hutauza kitu. ‎ ‎Unajua inakera kiasi gani kuandika post kali, halafu hakuna mtu ana-comment? ‎ ‎Halafu mtu mwingine anaandika tu: ‎"Siku zote pesa ziko mitaani." ‎Anapiga emoji 3 za moto. ‎Anapata likes 400. ‎ ‎Inakuchoma roho. ‎Unajisikia umechemka. ‎ ‎Unajiuliza, “Kwani shida iko wapi?” ‎ ‎Shida iko kwenye kichwa cha habari. ‎Hicho ndo mtego. ‎ ‎Na mtego ukikosa chambo, samaki hawezi kung’ang’ania. ‎ ‎ ‎Sasa sikia kaka/dada... ‎Kichwa cha habari siyo tu sentensi ya mwanzo. ‎ ‎Ni mlango...