Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya copywriting kupata mteja mafanikio ya mtaani kuandika matangazo kazi ya kalamu mteja wa kwanza maisha ya copywriter

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Hivi Ndivyo Nilivyopata Mteja Wangu Wa Kwanza Kwa Kalamu Tu!...

Picha
  ‎ ‎Kakaa/Dadaa yangu… ‎ ‎Hivii ushawahi kukaa na njaa hadi unaandika mawazo kwenye daftari badala ya kula? ‎ ‎Mimi nilishawahi. ‎ ‎Nilikuwa na ndoto ya kuwa copywriter. ‎Lakini sikujua nianzie wapi. ‎ ‎Zero network. ‎Zero pesa. ‎Na mbaya zaidi… ‎ ‎Watu hawakuamini kitu kama *kuandika matangazo* ni kazi. ‎ ‎Walinicheka. ‎Hawakuziamini ndoto zangu. ‎Wengine walinambia: ‎ ‎"We kaa tu uandike mashairi yako huko!" ‎ ‎Nilihisi kama naota ndoto ambayo haipo kwenye Google. ‎Lakini moyo haukukubali niachane nayo. ‎ ‎Ilikuwa Kama Ndoto Mbaya ‎ ‎Kila siku nilikuwa ninaamka asubuhi na kuchora matangazo kwenye daftari la zamani. ‎ ‎Hapo.... ‎ ‎Sina laptop. ‎Sina printer. ‎Nina tu kalamu ya cello na daftari la kasuku. ‎ ‎Nilijifunza kuandika matangazo yenye hisia. ‎Yale ya kumgusa mtu mpaka ashindwe kulala bila kukutafuta. ‎ ‎Lakini bado… ‎Hakuna mtu aliyekuwa anajua kuwa mimi ni copywriter. ‎ ‎Nilikuwa kivuli. ‎ ‎Hapo Ndo Nikapiga Stop ‎ ‎Nikajikumbusha ile kauli niliyoambiwaga na mento...