Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya maisha bila kusoma

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Unakufa Taratibu… Bila Hata Kujua Sababu? HUJISOMEI!

  ‎‎Unajua nini kaka/dada…  Kuna maumivu huwa hayapigi kelele. ‎Hayaleti presha. Hayajulikani fasta. ‎Yanakuja polepole… kimyakimya… mpaka siku moja unajikuta umepotea kabisa. ‎ ‎Na moja ya maumivu hayo ni… ‎Maisha Bila Kusoma Vitabu. ‎ ‎Soma hapa sasa: ‎Watu wengi wanaishi kama vile kusoma ni kwa ajili ya shule tu. ‎Au ni kitu cha wasomi. ‎Au ni “luxury” ya watu wanaotafuta PhD. ‎ ‎Lakini ukweli ni huu: ‎Maisha Bila Kusoma ni kama gari bila mafuta. ‎Unalipenda. Unalipiga mswaki kila asubuhi. ‎Lakini halisogei. ‎Linasimama pale pale, siku baada ya siku. ‎ ‎Umeshajiuliza kwanini maisha yako yamekuwa magumu hivi? ‎Kwanini kila mwaka una malengo… lakini hakuna kinachobadilika? ‎ ‎Kwanini wengine wanakimbia… na wewe unatembea? ‎Au hata kutambaa ni kazi? ‎ ‎Ni kama dunia inasonga mbele… lakini wewe umesahaulika. ‎Unajituma. Unahangaika. ‎Lakini bado maisha hayakusikilizi. ‎ ‎Na wakati wewe unapiga miayo ukiangalia TikTok… ‎wengine wanasoma makala, vitabu, kozi, wanajifunza skills… ...