Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya maendeleo ya akili

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Jinsi Kusoma Vitabu Kunavyobadilisha Ubongo Wako....

  ‎Rafiki Yangu, ‎ ‎Miaka michache iliyopita, nilikuwa mtu wa kawaida sana. ‎Nilikuwa na ndoto kubwa… lakini akili iliyochoka. ‎Kichwa kilijaa mazungumzo ya watu, si ndoto zangu. ‎Nilikuwa nikiamka asubuhi nikijiuliza, “Hivi akili yangu inafanya kazi kwa asilimia ngapi tu?” ‎ ‎Sikujua kuwa kitu kimoja kidogo kingeweza kubadilisha kabisa maisha yangu. ‎ ‎Siku moja, nikiwa napitia changamoto za maisha, nilikutana na kitabu kidogo cha kurasa 120. ‎Jina lake lilikuwa ni "Change Your Thinking Change Your Life” ‎ ‎Kwa dharau nikasema, “Kitabu gani hiki? Kitatofautisha nini?” ‎Lakini kuna sauti ndani yangu ilisema: ‎“Jaribu. Una nini cha kupoteza?” ‎ ‎Nilikubali… Nikaanza kusoma. ‎ ‎Mwanzo kilikuwa kigumu. Ubongo wangu ulitaka kuachana nacho. ‎Nilikuwa nimezoea starehe, sio maarifa. ‎Nilikuwa mwepesi wa kuangalia video, sio kusoma kurasa. ‎ ‎Lakini kwa namna ya ajabu  kila ukurasa niliomaliza, akili yangu iliongezeka nguvu. ‎Nilianza kuona vitu nilivyokuwa sivi...