Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Umekwama

‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

‎🔥 Story: Nilipochoka Kuishi Maisha Duni...

Safari Ya Kujiokoa Kwa Vitabu ‎ ‎Nakumbuka Miaka 9 iliyopita nilikuwa mtu wa "tutasonga tu." ‎Nilikuwa na maisha ya kawaida, kazi ya kawaida, ndoto za kawaida na hata mawazo ya kawaida. ‎ ‎Lakini moyoni… ‎Nilihisi kuna kitu nakikosa. ‎Nilikuwa hai, lakini si mzima. ‎Nilicheka, lakini ni kwa Kujilazimisha. ‎Niliamka kila siku, lakini bila msisimko. ‎ ‎Ilikuwa kama maisha yananipita tu na mimi nikiangalia kama mgeni. ‎ ‎ ‎Siku moja, nilikutana na rafiki mmoja wa zamani alikuwa tofauti. ‎Anang'ara. Anaongea kwa uthabiti. Ana maono. ‎ ‎Nikamwambia: ‎“Bro, umebadilika sana. Ulifanya nini?” ‎ ‎Akaniambia kwa upole, ‎“Niliamua kuanza kusoma vitabu sahihi. Ndipo maisha yangu yakaanza kubadilika polepole.” ‎ ‎Nikacheka kwa kejeli: ‎“Vitabu tu?” ‎ ‎Akaniambia, ‎“Ndiyo. Lakini si vitabu vyovyote. Vitabu vya kujijenga. Vitabu vya kuamka tena. Vitabu vya kujikomboa.” ‎ ‎Nilirudi nyumbani nikiwa na changamoto kichwani. ‎Mimi? Kusoma vitabu? Mimi si mtu wa vitabu. ‎Niliona kama hiyo ni ...