Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kichwa cha habari

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Angalia Nguvu Ya Haya Maneno Matano (5) Yenye Kulevya – Maneno Yanayovutia Haraka Machoni.....

‎Rafiki Yangu Mpendwa, ‎ ‎Unajua shida kubwa ya wengi? ‎Wanaandika maneno ya kawaida mno. ‎Maneno yaliyokufa. ‎Hayana ladha. Hayagusi hisia. ‎Yanapitwa tu kama upepo. ‎ ‎Alafu wanashangaa... ‎Mbona hakuna anayesimama kusoma? ‎Mbona hakuna anayebonyeza? ‎ ‎Sasa leo nakuonyesha kitu kinono. ‎Maneno matano tu. ‎Lakini ni hatari. ‎Yana nguvu ya kuvuta macho ya mtu hata akiwa bize aje asome tu. ‎ ‎Hebu fikiria… ‎Umeweka post kali sana. ‎Unajua kabisa kuna madini. ‎Lakini hakuna mtu anaye-comment. ‎Hakuna likes. Hakuna saves. ‎ ‎Unakata tamaa. ‎Unaanza kufuta post zako. ‎Unaamini labda huwezi. ‎ ‎Unajua kwanini? ‎Ni kwa sababu kichwa cha habari yako kinapwaya. ‎ ‎Hakina mvuto. ‎Hakina “punch.” ‎Hakina kulevya. ‎ ‎Sikiliza kaka, dada... ‎Hili neno “karibu” ni zuri. ‎Lakini halina nguvu kama “karibu ujionee.” ‎Hili neno “soma” ni zuri. ‎ ‎Lakini halivutii kama “soma haraka kabla haijatolewa.” ‎ ‎Unashika pointi? ‎Lugha ya kuuza lazima iwe na mchele wa maneno ya moto. ‎Maneno ya kishindo. ‎Mane...

‎Sanaa Ya Kuandika Kichwa Cha Habari Cha Kutosha Kuusimamisha MOYO Wa MTEJA

‎“Ukishika hii, unaweza kuuza barafu jangwa la Sahara” ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu.... ‎Unajua shida kubwa ya waandishi wengi wa matangazo? ‎Wanahangaika kuandika miandiko mizuri sana… ‎ ‎Lakini "kichwa cha habari chao ni cha kawaida sana". ‎ ‎Halafu wanashangaa kwa nini hakuna anaye-click. ‎ ‎Wanasema watu hawasomi. ‎Hapana. ‎ ‎Watu wanasoma ‎Wanasoma vichwa vya habari tu. ‎ ‎Kama kichwa hakishiki moyo… ‎Kama hakimshtui mteja… ‎Kama hakimfanyi asimame hata kama alikuwa anaenda chooni… ‎ ‎Hutauza kitu. ‎ ‎Unajua inakera kiasi gani kuandika post kali, halafu hakuna mtu ana-comment? ‎ ‎Halafu mtu mwingine anaandika tu: ‎"Siku zote pesa ziko mitaani." ‎Anapiga emoji 3 za moto. ‎Anapata likes 400. ‎ ‎Inakuchoma roho. ‎Unajisikia umechemka. ‎ ‎Unajiuliza, “Kwani shida iko wapi?” ‎ ‎Shida iko kwenye kichwa cha habari. ‎Hicho ndo mtego. ‎ ‎Na mtego ukikosa chambo, samaki hawezi kung’ang’ania. ‎ ‎ ‎Sasa sikia kaka/dada... ‎Kichwa cha habari siyo tu sentensi ya mwanzo. ‎ ‎Ni mlango...