Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Jifunze mbinu rahisi ya kusoma vitabu dakika tano kila siku hata ukiwa na ratiba ngumu.

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Sina Muda Ni Uongo Unaouamini...

 Rafiki Yangu, Hii ni sababu Pekee Inayokuzuia Kusoma na Kubadilika. Kama huna dakika tano za kusoma leo, huna haki ya kulalamika kesho kwamba maisha yako hayajabadilika. Ni kauli maarufu sana miongoni mwa watu wa mtaani: *Mimi napenda kusoma, lakini sina muda.* Kila mara nikisikia mtu anasema hivyo, najua huyu hajawahi kuhesabu saa zake. Hebu fikiria, unapoamka asubuhi, hadi unapolala usiku, kweli hakuna dakika tano za bure? Hakuna muda wa kusubiri foleni kwenye daladala, benki, hakuna dakika ya kusubiri chakula kiive, hakuna muda wa dakika chache kabla ya kuingia kazini? Ukweli ni kwamba, muda upo, ila tunauharibu kwa kufanya mambo madogo madogo. Brian Tracy kwenye kitabu chake cha Eat That Frog First anasema:  Kama hutapanga muda wako, mtu mwingine atakupangia. Na ndiyo maana unaona siku inakimbia, halafu unabaki na hali ile ile mwaka hadi mwaka. Huu msemo wa sina muda ni uongo tuliojifundisha kuuamini ili kujisamehe kwa kutokuchukua hatua.  Ni kama ngao ya kujificha i...