Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya faida ya kurudia vitabu

‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

Ukweli Wa Kushangaza: Mara Ya Pili Nilipokisoma… Ndipo Nilipokisoma Kwa Mara Ya Kwanza.....

‎Je, unapaswa kusoma kitabu mara moja au mara nyingi?  ‎ ‎Hadithi hii itakupa jibu la moyo.... ‎ ‎Nilikuwa na orodha ndefu ya vitabu. ‎ ‎Niliamini mafanikio yangu yanategemea idadi ya vitabu nilivyomaliza. ‎ ‎Nikawa najisifu: “Nimesoma vitabu 12 mwaka huu!” ‎ ‎Lakini cha kushangaza, sikumbuki hata sura ya kwanza ya vitabu vitano. ‎ ‎Nilikuwa msomaji mwenye kasi, lakini si mwenye mabadiliko. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎Don’t just read more books. ‎ ‎ Reread the right ones. ‎ ‎Nukuu hiyo ilinichoma kama sindano ya kweli. ‎ ‎Nikajiuliza: “Ina maana nasoma sana lakini bado nipo palepale?” ‎ ‎Nilijitetea: ‎“Mbona kusoma kitabu mara moja tu inatosha?  ‎ ‎Sina muda wa kurudia! Kuna vitabu vingapi bado sijavifungua? ‎ ‎Niliona kurudia kitabu kama kurudia darasa uliokwisha kufaulu. ‎ ‎Lakini ndani kabisa, nilihisi kuna kitu kinakosekana. ‎ ‎Nikamkuta mjasiriamali mmoja aliyenukuliwa kwenye podcast: ‎.Mimi husoma vitabu vichache lakini kila mwaka narudia vitabu vitatu muhimu. ‎...