🔥 Nilikuwa Sina Dira... Mpaka Kitabu Kimoja Kilivyonibadilisha...
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Siku zote nilikuwa mtu wa kawaida tu.
Ninaamka asubuhi, nakwenda kazini, narudi jioni nikiwa nimechoka.
Mishahara ni ileile, ndoto zipo tu kichwani lakini hakuna kinachoenda mbele.
Nilihisi maisha hayaendi… lakini pia sikuamini sana mambo ya vitabu.
Nikajipa moyo: “Hivi kweli mtu anaweza kufanikiwa kwa kusoma tu?”
Siku moja nikiwa kwenye daladala, nikasikia kijana mmoja akimwambia mwenzake:
"Mimi sikuchaguliwa chuoni, lakini kitabu kimoja kilinifunulia njia.
Sasa nauza online na nimefungua biashara yangu."
Maneno yale yalinigusa kama mshale.
Je, nami naweza kubadilika kupitia kusoma?
Nilijitetea:
"Aah! Mbona wengi wanasoma hawafanikiwi? Wengine wanamaliza PhD lakini bado ni masikini."
Nikajifariji kwa kisingizio cha muda na pesa.
Lakini moyoni nilihisi sauti ikiniambia: "Jaribu. Hata kama ni mara moja."
Nikamfuata rafiki yangu mmoja, ambaye nilimjua ana maendeleo makubwa.
Alinitazama na kuniambia kwa sauti ya upole:
"Mafanikio huanza kichwani. Ukikitunza kichwa chako, maisha yatakusikiliza.
Anza na kitabu kimoja tu."
Akanipa kitabu cha “Think and Grow Rich.”
Nikaanza kusoma taratibu... bila shinikizo.
Nilipoanza kusoma, sikuamini macho yangu.
Nilianza kufikiria kwa njia tofauti.
Nikaanza kuandika ndoto zangu.
Nikaanza kutunza muda wangu.
Nikagundua, kumbe matatizo yangu mengi yalianzia kwenye namna ninavyofikiri.
Wengine walinizomea: "Eti unasoma vitabu? Si vitasaidia nini Tanzania hii?"
Wengine wakaniita ‘mjuaji’ au ‘philosopher’ wa mtaa.
Lakini nilivumilia.
Nikaanza kutafuta vitabu vingine.
Nikakutana na watu wenye mawazo chanya.
Tukaanzisha group la kujifunza pamoja.
Wakati mmoja nilivunjika moyo.
Baada ya kusoma na kujifunza sana, bado maisha yalikuwa magumu.
Nikaanza kujiuliza: "Je, hivi vitabu ni hadithi nzuri tu zisizo na faida halisi?"
Lakini nikakumbuka nukuu moja niliyoisoma:
"Watu huacha mita moja kabla ya dhahabu."
Nikaamua kuendelea.
Miaka miwili baadaye, nilianza biashara ndogo mtandaoni kwa kutumia maarifa niliyojifunza kutoka kwenye vitabu.
Nikaanza kupata faida.
Nikaanza kusaidia familia.
Nikaanza kufundisha wengine.
Nilirudi kwa wale waliokuwa wakinibeza.
Sikumsema yeyote.
Niliamua kuandika blogi, kushiriki video, na kusaidia vijana walio kama mimi wa zamani.
Nilitaka kuwapa zawadi ile ile niliyopata: Maarifa.
Leo, mimi si yule mtu wa zamani.
Sina tena hofu ya kesho.
Sina mashaka na ndoto zangu.
Nimejifunza kuwa vitabu si hadithi tu ni ramani ya maisha.
Mafanikio huanza kichwani, na vitabu ndio ufunguo wa kufungua kichwa.
Leo naandika hadithi hii kwa ajili yako.
Kama uko pale nilipokuwa mimi, usipuuze vitabu.
Usipuuze kujifunza.
Soma.
Jifunze.
Tumia.
Kama vilinibadilisha mimi, vinaweza kukubadilisha wewe pia.
Karibu tuungane Pamoja,
Tuwasiliane Kwa Namba 0750376891.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni