Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Jifunze jinsi ya kulenga wateja sahihi na kuongeza mauzo kwa kutumia mbinu za kisasa za mauzo na masoko.

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Usiuze Kwa Wote Wauzie Wanaokuhitaji Zaidi!... ‎

Rafiki, ‎ ‎Unapojaribu kumfurahisha kila mtu, unamkosa mtu sahihi ‎ ‎Mtu mmoja aliniambia, “Mimi nauza kila kitu kwa kila mtu.” ‎ ‎ Nikamuuliza, “Unapata wateja wangapi?” Akasema, “Wachache sana!” ‎ ‎Hapo ndipo nilimwambia ukweli mchungu: ‎ ‎ 👉 Biashara yako si kanisa la jumapili haipaswi kuwahubiria wote. ‎ ‎Ukiuza kwa kila mtu, unauza kwa hakuna mtu. ‎ ‎Unahitaji kuelewa ni nani unayemhitaji, unayemwelewa, na anayeona bidhaa zako kama suluhisho lake.  ‎ ‎Huyo ndiye mteja sahihi. ‎ ‎Katika somo hili utajifunza: ‎ ‎Kwa nini ni hatari kuu kuuza kwa kila mtu, ‎ ‎Jinsi ya kuwatambua wateja sahihi kwa biashara yako, ‎ ‎Mbinu 5 za kuvutia na kushikilia wateja waliolengwa vizuri, ‎ ‎Na jinsi ya kuacha watu “wasio wa kwako” bila kuathiri biashara yako. ‎ ‎Fikiria biashara yako ikiwa imejaa wateja unaowapenda, wanaokuelewa, wanaolipa kwa wakati, na wanaosambaza jina lako kwa wengine.  ‎ ‎Hutoi ofa ovyo, hutumii muda mwingi kuwashawishi kwa sababu tayari wanajua wanachokitafuta. ...