‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

Kwanini Wanaosoma Vitabu Huonekana Wasomi Zaidi? Siri Ambayo Wengi Hawajui! ‎

Hii Ndio Sababu Halisi Wengi Hawaijui!

‎Rafiki Yangu,

‎Unakutana na mtu hajavaa suti. Hana lafudhi ya kizungu.

‎Lakini ukiongea naye, anakuvutia. Anakuonesha dunia kwa maneno.

‎Unajiuliza, “Huyu kazitoa wapi hizi akili?”

‎Jibu ni rahisi anasoma vitabu.

‎Vitabu sio tu karatasi na maneno. Ni bunduki ya akili.

‎Ukivisoma, unajifunza kuongea kama mtaalam.

‎Unajua kuandika vizuri, kufikiri kwa undani, na kuelewa haraka mambo ambayo wengine bado wanashangaa.

‎Sasa angalia watu ambao hawasomi.

‎Wanaongea kama watu wa mitandaoni.

‎Wanaishi kwa maneno ya "nilisikia", "walisema", na "inavyoonekana".

‎Hawana msimamo.

‎Hawajui kwa nini wanafanya wanachofanya.

‎Wanadanganywa kirahisi.

‎Kila kitu kwao ni “trend”, si truth.

‎Na ukikaa nao, unahisi unarudi nyuma kimaendeleo.

‎Unadhani kusoma ni kazi ya shule?

‎Ama ni kwa watu waliopata division one?

‎Umeambiwa uache vitabu usije ukaonekana "unaringa"?

‎Huo ni uongo mkubwa kuliko ahadi za wanasiasa.

‎Mtu anaposoma vitabu, anachonga akili yake.

‎Anapata maneno ya kusema, hekima ya kutenda, na moyo wa kuelewa.

‎Sio lazima uende chuo.

‎Lakini ukisoma vitabu vizuri, unaweza kumfunza hata Profesa.

‎Anza kusoma vitabu.

‎Si lazima viwe vya kiingereza kigumu kama cha Shakespeare.

‎Anza na vitabu vya maisha, biashara, pesa, mahusiano.

‎Kila siku soma kurasa 5 tu.

‎Baada ya miezi 3, utagundua maneno yako yamebadilika.

‎Mtazamo wako umeinuka.

‎Hata watu wataanza kukuuliza, “Wewe ni msomi wa chuo gani?”

‎Hapo nyuma....

‎Nimekutana na kijana mmoja Kariakoo.

‎Anaitwa Jumanne, alikuwa anauza socks.

‎Kila muda wa mapumziko, alikuwa anasoma kitabu cha "Think and Grow Rich".

‎Nilimwambia, Hii kitu itakusaidia kweli

‎Aliniambia, “Mzee, akili haibebwi na elimu, inabebwa na maarifa.”

‎Miaka miwili baadae, nikamkuta anauza bidhaa mtandaoni.

‎Amesajili kampuni. Ana timu ya vijana 5.

‎Ameniambia, “Mkufunzi Ramadhani, kilichonitoa kwenye stendi sio hela  ni vitabu.”

‎Niliinama nikamwambia, “Wewe sasa ni msomi halisi.”

‎Unataka kuonekana msomi kweli?

‎Si lazima usome vitabu kumi kwa siku.

‎Anza na kimoja.

‎Jifunze. Badilika. Ishi kwa maarifa.

‎Ukitaka vitabu vya kukuchochea kwa lugha rahisi na ya maisha niambie.

‎ Nitakutumia mapendekezo.

‎Tuwasiliane NAMBA Ni 0750376891.

‎Maisha ni mafupi sana kuishi bila maarifa! 🧠🔥

‎Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan,

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?