Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Nguvu ya Vitabu

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Mtoto Wa Mchuuzi Aliyejijengea Ujasiri Kwa Kurasa...

 ‎Kijiji cha Msaranga kilijulikana kwa soko lake dogo lenye kelele nyingi na vumbi la kila asubuhi.  ‎ ‎Hapo ndipo alipokulia Amani, kijana mdogo, mtoto wa mchuuzi wa viazi. ‎ ‎Maisha yalikuwa magumu.  ‎ ‎Kila siku ilianza kwa sauti ya mama yake akimwamsha mapema: ‎ ‎“Amani, chukua ndoo, twende sokoni.” ‎ ‎Amani alikuwa mpole, mwenye aibu na asiyejiamini.  ‎ ‎Kila alipokuwa karibu na watu wengi, sauti yake ilikuwa ndogo kama ya kupiga dua moyoni.  ‎ ‎Alipoitwa darasani ajibu swali, alitetemeka. Watu walimcheka. Alijiona dhaifu. Akijisemea moyoni, ‎ ‎"Mimi siwezi kuwa kama wale watoto wanaoongea mbele za watu. Mimi si kitu." ‎ ‎Siku moja, akiwa anafagia meza sokoni, aliona karatasi la gazeti limefungiwa samaki.  ‎ ‎Katika lile karatasi, kulikuwa na maneno yaliomvutia: ‎ ‎ “Vitabu vinawafanya watu kuwa huru.” ‎ ‎Alishangaa. Akajiuliza, “Inawezekanaje kurasa tu zabadili maisha ya mtu?”  ‎ ‎Hapo ndipo moyo wake mdogo ukapata hamu ya kujua zaidi. ‎ ‎Lakini ...

‎Siri Ya Kusoma Vitabu Vingi Bila Kuvisahau.....

  ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Unasoma kitabu leo... kesho umesahau kila kitu. ‎Ushaona hiyo kitu? Inachosha. Inakatisha tamaa. ‎Unajikuta unasoma tu, lakini hamna unachobeba. ‎ ‎Kama umewahi kujisikia hivyo… karibu kwenye club yetu. ‎ ‎Lakini leo nataka nikuambie kitu cha maana sana. ‎Siri ambayo wengi hawajui. ‎Siri ya kusoma vitabu vingi bila kuvisahau. ‎Na kuvitumia kukuinua maishani. ‎ ‎ ‎Unasoma, unasahau. Unasoma, unasahau. ‎Kama vile ubongo wako unazima mara tu ukifunga kitabu. ‎Unajikuta unarejea kwenye maisha ya zamani. ‎ ‎Unasema “Aaah, kile kitabu kilikuwa kizuri sana…” ‎Lakini ukuliza ulijifunza nini? Unashindwa kusema. ‎ ‎Inaumiza. Sana. ‎Ni kama unakula chakula kizuri, lakini mwili wako haukipokei. ‎Hakuna nguvu. Hakuna mabadiliko. Hakuna matokeo. ‎ ‎Lakini tatizo si wewe. ‎Tatizo ni mbinu unayotumia. ‎Watu wengi husoma vitabu kama vile wanasoma gazeti. ‎ ‎Wanakimbia. Wanamaliza haraka. ‎Wanataka kumaliza kurasa nyingi bila kutafuna kilichoandikwa. ‎ ‎Halafu wanashanga...

Akili Kwanza Consultants - Ndoto Mpya Inayochipua Kutoka Nguvu Ya Vitabu

Picha
Muda si mrefu uliopita , nilianzisha blogu hii kwa jina “Nguvu Ya Vitabu” kwa lengo moja kuu: Kugusa akili za watu kupitia maarifa ya vitabu. Nilitamani kuona vijana, wafanyabiashara, na watu wa kawaida wakigundua hazina iliyofichwa ndani ya kurasa za maarifa. Lakini sasa… Ndani yangu inaanza kuchipua ndoto mpya, ndoto ya kupeleka maarifa haya mbali zaidi. Ndiyo maana leo natangaza rasmi kuanzishwa kwa mpango mpya uitwao: Akili Kwanza Consultants Kwa Nini Jina Hili? Nimechagua jina hili kwa sababu lina ujumbe mzito: Akili Kwanza – linaweka wazi kuwa hakuna maendeleo, mafanikio, au mabadiliko bila kuanza na mabadiliko ya fikra. Consultants – linaashiria kwamba tunakwenda mbali zaidi ya kutoa tu maarifa. Tunataka kusaidia watu kubadili maisha yao kupitia ushauri, mwelekeo, na mbinu za vitendo. Akili Kwanza Consultants Itasimamia Nini? Taasisi hii itajikita katika: Ushauri wa kimaendeleo (maisha, biashara, na maarifa) Ushauri kwa vijana na wanaoan...