Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya vitabu vs audiobook

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Kuna Tofauti Gani Kati ya Kusoma Vitabu Halisi na Audiobooks?

 ‎📘 Sauti Iliongea Nami… Ndipo Nikagundua Nguvu Halisi ya Kusoma ‎ ‎Mimi nilikuwa msomaji wa kawaida sana. ‎Nilipenda vitabu… lakini muda wa kusoma? Hakuna! ‎ ‎Kazi nyingi, kichwa kiliniuma jioni, mara simu, mara familia. ‎Vitabu vinanivutia lakini kuvisoma ni kama kujilazimisha. ‎Nikaanza kujisikia kama nimechoka kuwa na ndoto zisizoendelezwa. ‎ ‎Siku moja rafiki yangu akaniambia: ‎"Kama kusoma kunakuchosha, kwanini usijaribu audiobook?" ‎Nilicheka tu. ‎ ‎"Kusikiliza si sawa na kusoma!" Nikasema kwa kejeli. ‎ ‎Nilihisi kama nikisikiliza kitabu, nitakuwa mvivu. ‎"Hakuna mtu aliyefanikiwa kwa kusikiliza tu... ni kama kudesa!" ‎Niliendelea kung’ang’ania vitabu vya karatasi, lakini vingi vikasalia na vumbi kabatini. ‎ ‎Siku moja nikiwa YouTube, nikamuona mtu mashuhuri akisema: ‎"Audiobooks zimenisaidia kusoma zaidi ya vitabu 50 kwa mwaka." ‎ ‎Nikaguswa. Nikasema: ‎"Subiri kidogo… Huyu amefanikiwa, na anasikiliza vitabu? Labda kuna jambo hapa....