Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Faida 7 Za Kipekee Za Kusoma VITABU Kila Siku Hata Kama Ni DAKIKA 10 TU!

 ‎


‎Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Watu wengi wanalalamika hawafanikiwi.

‎Wanajitahidi sana lakini hakuna hatua zozote wanazopiga.

‎Wengine kila siku wako online lakini akili zao ziko offline.

‎Kila mtu anatafuta "shortcut ya mafanikio", lakini wanakosa kitu kimoja cha msingi...

‎Kusoma vitabu.

‎Ndiyo, hata kama ni dakika 10 tu kwa siku, inaweza kubadilisha kila kitu.

‎Hebu fikiria…

‎Miaka mitano ijayo, utakuwa mtu yule yule tu, isipokuwa tu kwa vitu viwili:

‎Vitabu ulivyosoma, na watu ulioambatana nao.

‎Sasa kama kila siku unasoma status, memes na story za watu…

‎Lakini huwezi kusoma hata ukurasa mmoja wa kitabu, unajidhulumu mwenyewe.

‎Mafanikio hayaji kwa kuomba omba—yanakuja kwa maarifa.

‎Na maarifa yapo vitabuni.

‎Ukikwepa kusoma leo, utajikuta unakumbana na matatizo yale yale kesho.

‎Kuna watu wanasema, “Mimi siwezi kusoma vitabu.”

‎“Nachoka haraka.”

‎"Usomaji sio vitu vyangu."

‎Wanajikosea sana.

‎Hakuna mtu yeyote aliyezaliwa akijua kusoma.

‎Lakini kila mtu anaweza kujifunza kupenda kusoma.

‎Na usidanganywe…

‎Huwezi pata mafanikio ya kweli kwa kusikiliza tu motivational videos.

‎Au kwa kubrowse quotes kila siku.

‎Vitabu vinakupa undani.

‎Vitabu vinakuza akili.

‎Vitabu vinakufungua kichwa.

‎Dakika 10 tu kwa siku, zinaweza kukuokoa na miaka 10 ya mateso.

‎Sasa hebu niambie, unawezaje kufaidika na kusoma vitabu kila siku?

‎Hii hapa orodha ya faida 7 zinazokukodolea macho:

‎1. Unakua Mwerevu Zaidi.

‎Unajua mambo mengi kuliko watu wa kawaida.

‎Unakuwa na hoja nzito. Unatisha kimawazo.

‎2. Unajiamini Sana.

‎Unapokuwa na maarifa, huogopi kusema.

‎Huogopi changamoto. Unasimama imara.

‎3. Mawazo Yako Yanakuwa Safi.

‎Vitabu vinasaidia akili yako kuwa tulivu.

‎Vinapunguza stress na msongamano wa mawazo.

‎4. Unaongeza Kumbukumbu na Umakini.

‎Kusoma ni kama kuufanyisha mazoezi ubongo.

‎Kadri unavyosoma, ndivyo unavyoimarika kiakili.

‎5. Unapata Mawazo Mapya Ya Biashara, Maisha na Mafanikio.

‎Kuna watu walifaulu kabla yako.

‎Waliandika walichojifunza.

‎Unapovisoma vitabu vyao unafupisha njia.

‎6. Lugha Yako Inaimarika.

‎Unaanza kuongea vizuri.

‎Kuandika vizuri. 

‎Kujieleza kwa ufasaha.

‎7. Unajitambua Zaidi.

‎Vitabu vinaangaza ndani yako.

‎Vinakufundisha kuhusu wewe mwenyewe.

‎Namkumbuka kaka mmoja mtaa wa Keko – anaitwa Ally.

‎Huyu jamaa aliwahi kuwa mchoma chips.

‎Lakini leo hii ni mtaalamu wa mitandao na ana biashara yake.

‎Niliuliza siri yake, akaniambia kitu kimoja:

‎“Niliamua kusoma kitabu kimoja kila mwezi. Hata kama ni ukurasa mmoja kwa siku.”

‎Kila kitu kilianza kubadilika.

‎Akili yake ikafunguka.

‎Akaanza kufikiri tofauti.

‎Leo hii, anawashauri wafanyabiashara wakubwa.

‎Si kwa sababu ya pesa aliyokuwa nayo bali maarifa aliyoyachota kwenye vitabu.

‎Sasa ni zamu yako.

‎Usisubiri kuwa na muda mwingi.

‎Anza na dakika 10 tu kwa siku.

‎Soma kabla ya kulala.

‎Soma ukiwa kwenye daladala.

‎Soma wakati wengine wanabishana kwenye comments.

‎Kumbuka:

‎Kila ukurasa unaosoma ni hatua moja karibu na ndoto zako.

‎Kama unahitaji vitabu bora vya kuanzia, niambie nitakushauri vizuri.

‎Andika Meseji *NATAKA VITABU*

‎Kwenda 0750376891.

‎Usikubali maisha yakutese kwa sababu hujachukua dakika 10 ya kujisomea.

‎Weka comment yako hapo chini…

‎ Umesoma kitabu gani mwezi huu?

‎Twende kazi!

‎Karibu.

‎0750376891.

‎Mkufunzi Ramadhan Amir

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection