Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya nidhamu na kujiamini—mambo ambayo hayafundishwi kabisa shuleni

‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi Wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu? ...

 ‎ Hii hapa safari ya kugusa moyo wako. ‎ ‎Nawezaje Kuwa Mwanafunzi wa Maisha Kupitia Kusoma Vitabu?.... ‎ ‎Nilikuwa nimehitimu shule. ‎ ‎Nikiwa na cheti mkononi na ndoto kubwa kichwani. ‎ ‎Lakini maisha yakaniambia: “Karibu kwenye darasa halisi.” ‎ ‎Sikupata kazi niliyoitegemea. ‎ ‎Nikawa najiuliza: "Kwani elimu yangu haikutosha?" ‎ ‎Nilikuwa nimefundishwa mambo ya darasani lakini si maisha. ‎ ‎Siku moja nikakutana na nukuu: ‎ ‎“Don’t let school interfere with your education.” — Mark Twain ‎ ‎Nikaanza kujiuliza: ‎ ‎"Je, kuna elimu nyingine zaidi ya vyeti? Elimu ya maisha?" ‎ ‎Nikapuuzia. ‎ ‎Nikajua vitabu vya darasani tu ndivyo vya maana. ‎ ‎Niliona vitabu vingine kama vya watu walioshindwa. ‎ ‎Mbona havifundishwi shuleni? ‎ ‎Mbona havijasheheni nadharia na mitihani? ‎ ‎Mtu mmoja akanishika begani na kuniambia: ‎ ‎"Unapokoma kuwa mwanafunzi, ndipo unapokoma kukua." ‎ ‎Akanipa kitabu cha “Rich Dad Poor Dad.” ‎ ‎Akaniongeza na kingine:  ‎ ‎“The 7 Habits of ...

‎🔥 Mambo 7 Unayojifunza Kwenye Vitabu Ambavyo Hukufundishwa SHULENI 🔥...

  ‎Alizaliwa na Kuishi Maisha ya Kawaida Sana… ‎Anaitwa Jumanne. Mtoto wa pili kwenye familia ya watoto saba. Baba mchomeaji vyuma, mama muuza maandazi.  ‎ ‎Aliishi maisha ya kujisitiri, hakuwa na nguo za bei, wala viatu vya kuvutia. ‎ ‎ Alipomaliza kidato cha nne, hakupata nafasi ya kuendelea na masomo si kwa sababu hakufaulu, bali kwa sababu hakukuwa na ada. ‎ ‎Akiwa nyumbani, kila siku ilimchoma moyo kuona wenzake wakisonga mbele. Hakukuwa na ajira, wala mtu wa kumshika mkono.  ‎ ‎Ndoto zake zilianza kuzama polepole. Alianza kuamini pengine maisha haya ni ya waliozaliwa na bahati. ‎ ‎Lakini Mambo Yalianza Kubadilika Siku Aliyopewa Kitabu Kimoja. ‎Siku moja, jirani yake alimpa kitabu kiitwacho NGUVU YA VITABU. ‎ ‎“Jaribu kusoma hiki Kitabu,” alisema yule jirani, “Hata kama huendi shule, akili yako bado inaweza kuelimika.” ‎ ‎Kwa mashaka na shingo upande, Jumanne alianza kusoma. Kurasa za kwanza zilimkumbusha thamani ya muda, nguvu ya kujifunza, na umuhimu wa nidhamu bin...