Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya kuleta wateja

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Kwanini Wateja Hawaji? Dhana Potofu Unazozikumbatia Bila Kujua

‎Lucas alikuwa kijana mchanga aliyekuwa na ndoto kubwa ya kuwa mfanyabiashara maarufu jijini Arusha. ‎ ‎Alifungua duka la vifaa vya simu aliweka bidhaa mezani, akapamba maduka, akachapisha vipeperushi, na kila asubuhi aliingia mapema kwa matumaini. ‎ ‎Lakini mwezi ukapita, kisha mwingine. ‎ ‎Hakukuwa na wateja wa kutosha. Alianza kujiuliza: ‎ ‎"Ninajitahidi, mbona wateja hawaonekani?" ‎ ‎Siku moja, akiwa amekaa nje ya duka akiwa amechoka, mzee mmoja mtaalamu wa biashara alikuja na kumwambia: ‎ ‎“Una bidhaa nzuri, lakini si kila anayepita anajua hilo. ‎ ‎Tatizo si bidhaa zako, bali imani zako kuhusu wateja.” ‎ ‎Maneno yale yalimgonga kama radi. ‎ ‎ Lucas hakuwa amewahi kufikiri kuwa kuna dhana potofu zinazomzuia. ‎ ‎Lucas alicheka kwa kutoamini: ‎"Mzee, mimi nimesoma YouTube kila usiku, nimefanya kila kitu!" ‎ ‎Alijisemea: ‎ ‎"Labda biashara haijapangwa kwa ajili yangu. ‎ ‎Labda watu wa Arusha hawapendi kununua...