Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mafanikio

‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Niliwahi Kukimbizana na Wateja Kama Mwizi... Mpaka Copywriting Ilipoingia Maishani.

Picha
  ‎ Kakaa/Dadaa.... ‎ ‎Miaka michache iliyopita... ‎ ‎Nilikuwa ni yule jamaa anayekimbizana na wateja hadi kwenye inbox zao. ‎ ‎Natumia muda, nguvu, na data halafu wananipa “Nipo bize bro, nitakujulisha.” ‎ ‎Maumivu yake si mchezo. ‎ ‎Nilikuwa na bidhaa nzuri sana, lakini wateja walikuwa wagumu kama kokoto. ‎ ‎Nilijikuta najiuliza: ‎ ‎*Kwani lazima kuuza mpaka unatetemeka?* ‎ ‎*Kwanini wao wasikukimbilie kama wanavyokimbilia ofa?* ‎ ‎Niliona watu wengine wanaingiza mkwanja bila hata kuwa na bidhaa bora kuliko yangu. ‎ ‎Nikaanza kuhisi labda mimi ndo tatizo. ‎ ‎Lakini kumbe... ni lugha niliyokuwa natumia. ‎ ‎Wengi tunafikiri kuwa kupata wateja ni kuwa na bei ya chini au kutoa ofa. ‎ ‎Lakini ukweli ni huu: ‎ ‎Watu hawanunui bidhaa... Wananunua hisia. ‎ ‎Na hisia zinakuja kwa kutumia lugha ya kuwagusa. ‎ ‎Hapo ndipo nilipogundua nguvu ya copywriting uandishi wa matangazo yanayobeba roho. ‎ ‎Nikajifunza copywriting. ‎ ‎Nikaanza kuandika post fupi fup...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Picha
Kaka/Dada.... ‎ ‎Unawaza kuanzisha ndoto yako, labda ni  biashara, brand, au huduma fulani, ‎ ‎Lakini kila mara unaambulia jibu moja tu: *Huna mtaji!*  Au mbaya zaidi,  ‎ ‎*Wewe nani atakusaidia bila connection?* ‎ ‎Aisee, hii ni changamoto kubwa sana kwa vijana wengi mtaani, hususani wale waliokuwa na ndoto kubwa lakini mifuko yao haina hata mia.  ‎ ‎Na nilikuwa mmoja wao. ‎ ‎Ni kama maisha yanakuchokoza.  ‎ ‎Una wazo zuri kichwani, lakini kila ukiamka asubuhi, unashtukia huna hela ya kula, deni linagonga, halafu mtu anakwambia,  ‎ ‎*Ndoto haziliwi.* ‎ ‎Unajikuta unaanza kuamini labda kweli ndoto ni kwa matajiri tu.  ‎ ‎Unaacha kujaribu, unaweka ndoto zako ndani ya kabati, unarudi kutafuta ajira zisizo na roho, mradi tu uishi. ‎ ‎Lakini moyoni… unajua kabisa una kitu cha kipekee.  ‎ ‎Kinachokuuma si kwamba huwezi ni kwamba hujui wapi pa kuanzia bila pesa wala watu wa kukuvuta juu. ‎ ‎Hapa ndipo wengi wanakosea. ‎ ‎ Wanadhani kuwa mtaji wa pesa nd...