Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya tabia ya kusoma

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Nilikuwa Naogopa Kila Kitu… Mpaka Niliposoma Kitabu Kimoja Tu...

 Miaka ya nyuma, Mariam alikuwa binti mwenye ndoto kubwa, lakini mwenye sauti ndogo sana mbele ya watu. ‎ ‎Kila alipokuwa na wazo, moyo wake ulitetemeka kusema. ‎ ‎Kila alipohitaji kuongea mbele ya kundi, hata marafiki tu, alinyamaza. ‎ ‎Alikuwa anajilaumu kimya kimya: ‎“Mbona naona kila mtu ana ujasiri isipokuwa mimi?” ‎ ‎Siku moja, alihudhuria kikao cha wanawake wajasiriamali. ‎ ‎Mwanamke mmoja akasimama na kuongea kwa ujasiri wa kuvutia. ‎ ‎Baada ya mkutano, Mariam akamwendea kwa woga na kumuuliza: ‎ ‎"Ulikuwa na ujasiri mkubwa! Siri yako ni nini?" ‎ ‎Akamjibu kwa tabasamu: ‎“Nilianza kusoma vitabu. Si vitabu vya shule, bali vya maisha.” ‎ ‎Mariam alitabasamu tu na kusema kwa sauti ya chini: ‎"Mimi siwezi kuwa msomaji. Nikiwaza tu kurasa kumi, nashikwa na usingizi." ‎ ‎Lakini moyo wake haukutulia. ‎Usiku ule alitafakari: ‎"Kama kusoma vitabu kunabadilisha watu labda na mimi nitaweza." ‎ ‎Siku iliyofuata, alitumiwa link ya kujiunga na group la WhatsApp. ...

Mtoto Wa Mchuuzi Aliyejijengea Ujasiri Kwa Kurasa...

 ‎Kijiji cha Msaranga kilijulikana kwa soko lake dogo lenye kelele nyingi na vumbi la kila asubuhi.  ‎ ‎Hapo ndipo alipokulia Amani, kijana mdogo, mtoto wa mchuuzi wa viazi. ‎ ‎Maisha yalikuwa magumu.  ‎ ‎Kila siku ilianza kwa sauti ya mama yake akimwamsha mapema: ‎ ‎“Amani, chukua ndoo, twende sokoni.” ‎ ‎Amani alikuwa mpole, mwenye aibu na asiyejiamini.  ‎ ‎Kila alipokuwa karibu na watu wengi, sauti yake ilikuwa ndogo kama ya kupiga dua moyoni.  ‎ ‎Alipoitwa darasani ajibu swali, alitetemeka. Watu walimcheka. Alijiona dhaifu. Akijisemea moyoni, ‎ ‎"Mimi siwezi kuwa kama wale watoto wanaoongea mbele za watu. Mimi si kitu." ‎ ‎Siku moja, akiwa anafagia meza sokoni, aliona karatasi la gazeti limefungiwa samaki.  ‎ ‎Katika lile karatasi, kulikuwa na maneno yaliomvutia: ‎ ‎ “Vitabu vinawafanya watu kuwa huru.” ‎ ‎Alishangaa. Akajiuliza, “Inawezekanaje kurasa tu zabadili maisha ya mtu?”  ‎ ‎Hapo ndipo moyo wake mdogo ukapata hamu ya kujua zaidi. ‎ ‎Lakini ...

‎Kwa Nini Unaacha Kusoma Kitabu Kwenye Ukurasa wa 17? Hii Ndio Sababu Halisi (Na Inashangaza!)

Kwa Nini Ni Vigumu Kusoma Vitabu Mpaka Mwisho? ‎ ‎Kuna jamaa mmoja... ‎Anaitwa Musa Mfalme. ‎ ‎Sio mfalme kweli, lakini akili zake zilikuwa na hazina ya kifalme. ‎Alikuwa na ndoto kubwa sana. ‎Alitaka kuwa tajiri. ‎Mwenye maarifa. ‎Awe mtu wa tofauti. ‎ ‎Siku moja akapata kitabu. ‎Kikubwa. ‎Kimeandikwa kwa rangi ya dhahabu. ‎Juu yake kimeandikwa, ‎“Nguvu Ya Maarifa: Jinsi Ya Kujenga Maisha Yako Kuanzia Sasa.” ‎ ‎Akasema, ‎"Hili ndilo lililokuwa linanikimbia. Leo naanza, mpaka mwisho!" ‎ ‎Akasoma ukurasa wa kwanza. ‎Ukurasa wa pili. ‎Wa tatu... ‎Kichwa kinamwambia, “Bora uangalie TikTok kidogo tu…” ‎ ‎Akachukua simu. ‎Dakika mbili. ‎Zikawa saa moja. ‎Akasema, ‎"Kesho nitaendelea kusoma." ‎ ‎Hakurudi tena kwenye kile kitabu. ‎Mpaka leo. ‎ ‎Lakini Kwa Nini? Kwa Nini Tunashindwa Kumaliza Vitabu? ‎ ‎Hii hapa safari ya ukweli... ‎Safari ambayo Musa Mfalme alipitia na labda na wewe pia. ‎ ‎1. Vitabu Vinataka Nguvu Ya Ndani ‎ ‎Kusoma si kama kuangalia movie. ‎Hakuna kelele....

‎Jinsi Kusoma Vitabu Kunavyobadilisha Ubongo Wako....

  ‎Rafiki Yangu, ‎ ‎Miaka michache iliyopita, nilikuwa mtu wa kawaida sana. ‎Nilikuwa na ndoto kubwa… lakini akili iliyochoka. ‎Kichwa kilijaa mazungumzo ya watu, si ndoto zangu. ‎Nilikuwa nikiamka asubuhi nikijiuliza, “Hivi akili yangu inafanya kazi kwa asilimia ngapi tu?” ‎ ‎Sikujua kuwa kitu kimoja kidogo kingeweza kubadilisha kabisa maisha yangu. ‎ ‎Siku moja, nikiwa napitia changamoto za maisha, nilikutana na kitabu kidogo cha kurasa 120. ‎Jina lake lilikuwa ni "Change Your Thinking Change Your Life” ‎ ‎Kwa dharau nikasema, “Kitabu gani hiki? Kitatofautisha nini?” ‎Lakini kuna sauti ndani yangu ilisema: ‎“Jaribu. Una nini cha kupoteza?” ‎ ‎Nilikubali… Nikaanza kusoma. ‎ ‎Mwanzo kilikuwa kigumu. Ubongo wangu ulitaka kuachana nacho. ‎Nilikuwa nimezoea starehe, sio maarifa. ‎Nilikuwa mwepesi wa kuangalia video, sio kusoma kurasa. ‎ ‎Lakini kwa namna ya ajabu  kila ukurasa niliomaliza, akili yangu iliongezeka nguvu. ‎Nilianza kuona vitu nilivyokuwa sivi...