‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Unakufa Taratibu… Bila Hata Kujua Sababu? HUJISOMEI!

 

‎‎Unajua nini kaka/dada… 


Kuna maumivu huwa hayapigi kelele.

‎Hayaleti presha. Hayajulikani fasta.

‎Yanakuja polepole… kimyakimya… mpaka siku moja unajikuta umepotea kabisa.

‎Na moja ya maumivu hayo ni…

‎Maisha Bila Kusoma Vitabu.

‎Soma hapa sasa:

‎Watu wengi wanaishi kama vile kusoma ni kwa ajili ya shule tu.

‎Au ni kitu cha wasomi.

‎Au ni “luxury” ya watu wanaotafuta PhD.

‎Lakini ukweli ni huu:

‎Maisha Bila Kusoma ni kama gari bila mafuta.

‎Unalipenda. Unalipiga mswaki kila asubuhi.

‎Lakini halisogei.

‎Linasimama pale pale, siku baada ya siku.

‎Umeshajiuliza kwanini maisha yako yamekuwa magumu hivi?

‎Kwanini kila mwaka una malengo… lakini hakuna kinachobadilika?

‎Kwanini wengine wanakimbia… na wewe unatembea?

‎Au hata kutambaa ni kazi?

‎Ni kama dunia inasonga mbele… lakini wewe umesahaulika.

‎Unajituma. Unahangaika.

‎Lakini bado maisha hayakusikilizi.

‎Na wakati wewe unapiga miayo ukiangalia TikTok…

‎wengine wanasoma makala, vitabu, kozi, wanajifunza skills…

‎na wanachukua fursa zako. Ndiyo!

‎Wanachukua FURSA Zako LIVE!

‎Wengi hudhani pesa hupatikana kwa kuwa tu mchapakazi.

‎Eti ukiamka mapema na kulala late… utapiga hela.

‎Mbona mlinzi wa duka analala saa nane za usiku?

‎Mbona mama ntilie anachemsha maharage saa kumi alfajiri?

‎Sio kazi tu kaka…

‎Ni akili. 

‎Ni maarifa. 

‎Ni mbinu. 

‎Ni kusoma.

‎Kusoma kunakupa miwani ya kuona pesa mahali wengine hawaioni.

‎Kusoma kunakufungua akili, kinoma.

‎Kusoma kunakuonyesha shortcut halali.

‎Unataka kuanza kuona mabadiliko ya kweli?

‎Unataka pesa ianze kukuona?

‎Unataka kutoka kule kubaya uliko?

‎Jisomee.

‎Na siyo lazima usome vitabu vigumu kama sheria.

‎Anza na makala kama hii.

‎Anza na kurasa moja kwa siku.

‎Anza na kitu kinachohusu maisha yako moja kwa moja, pesa, mahusiano, biashara, mawasiliano, akili ya mtu mzima.

‎Kila ukurasa unakosoma… unakukomboa.

‎Mimi mwenyewe nilikuwa sina time na kusoma.

‎Nilidhani *mimi ni mwerevu tu wa kuzaliwa.*

‎Eti akili inatosha.

‎Nilikuwa na kiburi ya kijinga.

‎Mpaka siku moja nilikosa kazi… sababu tu niliulizwa swali la kawaida kwenye interview ,nikashindwa.

‎Swali lilikuwa kwenye kitabu nilichowahi kukiona… nikapuuza.

‎Nikaanza kusoma… polepole.

‎Leo hii, nimeandika makala hii, na unaisoma.

‎Najua kuandika kwa kuvuta hisia.

‎Najua kuuza kwa maneno.

‎Najua kuishi kwa akili, si jasho tu.

‎Yote… kwa sababu nilianza kusoma vitabu.

‎Maisha ni kama mtihani usio na tarehe ya kuanza.

‎Kama hutasoma… utaendelea kufeli.

‎Usikubali maisha yakupite tu.

‎Chukua hatua leo.

‎Jisomee.

‎Jifunze.

‎Jikomboe.

‎Maana kama hutajifunza leo…

‎Kesho itakugharimu zaidi.

‎Kama Unataka Kushirikiana Na Wenzako Kwenye Safari Hii Ya Usomaji Wa Vitabu,

‎Basi Tuma Ujumbe,

‎*NATAKA KUSOMA VITABU*

‎Kwenda 0750376891.

‎Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?