Machapisho

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Unakufa Taratibu… Bila Hata Kujua Sababu? HUJISOMEI!

  ‎‎Unajua nini kaka/dada…  Kuna maumivu huwa hayapigi kelele. ‎Hayaleti presha. Hayajulikani fasta. ‎Yanakuja polepole… kimyakimya… mpaka siku moja unajikuta umepotea kabisa. ‎ ‎Na moja ya maumivu hayo ni… ‎Maisha Bila Kusoma Vitabu. ‎ ‎Soma hapa sasa: ‎Watu wengi wanaishi kama vile kusoma ni kwa ajili ya shule tu. ‎Au ni kitu cha wasomi. ‎Au ni “luxury” ya watu wanaotafuta PhD. ‎ ‎Lakini ukweli ni huu: ‎Maisha Bila Kusoma ni kama gari bila mafuta. ‎Unalipenda. Unalipiga mswaki kila asubuhi. ‎Lakini halisogei. ‎Linasimama pale pale, siku baada ya siku. ‎ ‎Umeshajiuliza kwanini maisha yako yamekuwa magumu hivi? ‎Kwanini kila mwaka una malengo… lakini hakuna kinachobadilika? ‎ ‎Kwanini wengine wanakimbia… na wewe unatembea? ‎Au hata kutambaa ni kazi? ‎ ‎Ni kama dunia inasonga mbele… lakini wewe umesahaulika. ‎Unajituma. Unahangaika. ‎Lakini bado maisha hayakusikilizi. ‎ ‎Na wakati wewe unapiga miayo ukiangalia TikTok… ‎wengine wanasoma makala, vitabu, kozi, wanajifunza skills… ...

Mbona Unataka Kunilazimisha KUSOMA? Hii Ndio Siri Ya Kusoma Bila Kujiumiza!

  ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Kuna Watu Hupenda Kusoma Sana. ‎Wakiamka wanasoma. ‎Wakikula wanasoma. ‎Wakipanda gari wanasoma. ‎ ‎Lakini wewe? ‎Ukisikia neno “soma” unaona stress inakuja kama mawingu meusi. ‎ ‎Lakini sio kosa lako. ‎Uliwahi kulazimishwa kusoma. ‎Ulikaa darasani ukiangalia saa isogee. ‎Ukasoma ili ufaulu, si kwa sababu unataka. ‎ ‎Unajua Tatizo Liko Wapi? ‎Watu wanakudanganya eti: ‎*Tengeneza ratiba ya kusoma.* ‎ ‎Hawakuambii namna ya kuitengeneza ambayo haiwezi kukutesa. ‎Wewe si robot. ‎ ‎Wewe ni binadamu mwenye moods, pressure, akili na miguno. ‎ ‎Hebu Acha Hizi Ratiba Zenye Vifungo Kama Magereza. ‎ ‎Soma saa mbili hadi saa nne kila siku? ‎Saa tano asubuhi uanze na kitabu kizito? ‎Hapana. ‎Sio kila mtu anaweza hivyo. ‎ ‎Sasa Hebu Tujifunze Tofauti. ‎Kwanza, angalia maisha yako. ‎Wewe huamka saa ngapi? ‎ ‎Unakaa kwenye foleni? ‎Una muda wa kuscroll TikTok? ‎ ‎Hapo ndo panaitwa nafasi. ‎Usibadili maisha kwa ajili ya kusoma. ‎Ba...

‎Angalia Nguvu Ya Haya Maneno Matano (5) Yenye Kulevya – Maneno Yanayovutia Haraka Machoni.....

‎Rafiki Yangu Mpendwa, ‎ ‎Unajua shida kubwa ya wengi? ‎Wanaandika maneno ya kawaida mno. ‎Maneno yaliyokufa. ‎Hayana ladha. Hayagusi hisia. ‎Yanapitwa tu kama upepo. ‎ ‎Alafu wanashangaa... ‎Mbona hakuna anayesimama kusoma? ‎Mbona hakuna anayebonyeza? ‎ ‎Sasa leo nakuonyesha kitu kinono. ‎Maneno matano tu. ‎Lakini ni hatari. ‎Yana nguvu ya kuvuta macho ya mtu hata akiwa bize aje asome tu. ‎ ‎Hebu fikiria… ‎Umeweka post kali sana. ‎Unajua kabisa kuna madini. ‎Lakini hakuna mtu anaye-comment. ‎Hakuna likes. Hakuna saves. ‎ ‎Unakata tamaa. ‎Unaanza kufuta post zako. ‎Unaamini labda huwezi. ‎ ‎Unajua kwanini? ‎Ni kwa sababu kichwa cha habari yako kinapwaya. ‎ ‎Hakina mvuto. ‎Hakina “punch.” ‎Hakina kulevya. ‎ ‎Sikiliza kaka, dada... ‎Hili neno “karibu” ni zuri. ‎Lakini halina nguvu kama “karibu ujionee.” ‎Hili neno “soma” ni zuri. ‎ ‎Lakini halivutii kama “soma haraka kabla haijatolewa.” ‎ ‎Unashika pointi? ‎Lugha ya kuuza lazima iwe na mchele wa maneno ya moto. ‎Maneno ya kishindo. ‎Mane...

‎Kitabu Bora Kwa Mwanafunzi, Mjasiriamali Na Mfanyakazi– Usipite Bila KUKISOMA! ‎

‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Kuna tatizo kubwa sana. ‎Watu wanahangaika mchana kutwa. ‎Wanachoka. ‎Wanakatishwa tamaa. ‎Wanakazana ila pesa hazitoshi. ‎ ‎Unasoma hadi usingizi unakukataa, lakini bado maisha hayaeleweki. ‎Unafanya biashara, lakini kila siku unaishia na mia tano. ‎ ‎Umeajiriwa ,mshahara unamalizika kabla mwezi haujaanza. ‎ ‎Tatizo sio wewe. ‎Sio akili zako. ‎Tatizo ni kwamba… haujasoma kitabu hiki. ‎ ‎Kitabu kinaitwa "Nguvu Ya Buku" ‎Ni mwongozo mkali. ‎Umejaa mbinu. ‎Umejaa akili. ‎Umejaa moto. ‎ ‎Hebu jiulize… ‎Umeamka saa 11 alfajiri. ‎Umeenda kazini. ‎Umerudi jioni umechoka. ‎Kesho, unaamka tena… bila hata buku mfukoni. ‎ ‎Umewahi kujiuliza, hii ni maisha au ni kifungo? ‎Umewahi kujiangalia na kusema, “Naishi kweli?” ‎ ‎Huna amani. ‎Huna furaha. ‎Kila siku unajua lazima ukopeshane hadi mishahara. ‎ ‎Au utembee na deni la M-Pesa kama vile ni bangili. ‎ ‎Ni wakati wa kubadilika. ‎Na huwezi kubadilika bila maarifa. ‎Na maarifa hayaji tu, yananunuliwa. ‎ ‎Watu we...

‎Sanaa Ya Kuandika Kichwa Cha Habari Cha Kutosha Kuusimamisha MOYO Wa MTEJA

‎“Ukishika hii, unaweza kuuza barafu jangwa la Sahara” ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu.... ‎Unajua shida kubwa ya waandishi wengi wa matangazo? ‎Wanahangaika kuandika miandiko mizuri sana… ‎ ‎Lakini "kichwa cha habari chao ni cha kawaida sana". ‎ ‎Halafu wanashangaa kwa nini hakuna anaye-click. ‎ ‎Wanasema watu hawasomi. ‎Hapana. ‎ ‎Watu wanasoma ‎Wanasoma vichwa vya habari tu. ‎ ‎Kama kichwa hakishiki moyo… ‎Kama hakimshtui mteja… ‎Kama hakimfanyi asimame hata kama alikuwa anaenda chooni… ‎ ‎Hutauza kitu. ‎ ‎Unajua inakera kiasi gani kuandika post kali, halafu hakuna mtu ana-comment? ‎ ‎Halafu mtu mwingine anaandika tu: ‎"Siku zote pesa ziko mitaani." ‎Anapiga emoji 3 za moto. ‎Anapata likes 400. ‎ ‎Inakuchoma roho. ‎Unajisikia umechemka. ‎ ‎Unajiuliza, “Kwani shida iko wapi?” ‎ ‎Shida iko kwenye kichwa cha habari. ‎Hicho ndo mtego. ‎ ‎Na mtego ukikosa chambo, samaki hawezi kung’ang’ania. ‎ ‎ ‎Sasa sikia kaka/dada... ‎Kichwa cha habari siyo tu sentensi ya mwanzo. ‎ ‎Ni mlango...

‎Vitabu 3 Vilivyomtoa Huyu Kwenye Umaskini Kabisa Mpaka Kuwa Milionea

‎Bro! ‎Yani kuna kipindi alikuwa hana hata buku ya vocha. ‎Hana biashara. ‎Hana network. ‎Hana tumaini. ‎Alikuwa anapambana na maisha bila silaha. ‎Mtaa unamjua kama yule jamaa wa "bado tu". ‎Lakini sasa hivi? ‎Anaeza kukodi ndege. ‎Na anadai, vitabu vitatu tu ndiyo vilimtoa huko alikokuwa. ‎ ‎Watu wengi wako hoi. ‎Kazi ni kutafuta hela. ‎Hela yenyewe haikai. ‎Kila siku ni mipango, lakini hakuna kinachotoka. ‎ ‎Na tatizo kubwa ni hili: ‎Hawajui wanachokosa ni maarifa. ‎ ‎Unasikia mtu anasema: ‎"Hela ipo, mimi sina tu connection." ‎Au ‎"Sisi huku hatujapangiwa kuwa matajiri." ‎Aisee, hiyo ni uongo. ‎ ‎ ‎Kama hujui kutengeneza hela. ‎Na hujui kuitunza. ‎Halafu bado unaidai dunia ikutendee haki? ‎ ‎Kuna mtu mmoja alisema: ‎ ‎"Ukiwa maskini na bado hujifunzi, unajitakia." ‎ ‎Inaumiza lakini ni ukweli. ‎Maisha hayaoni huruma. ‎Ni ya wale wanaojua. ‎ ‎Wanaojifunza. ‎Wanaojichukua serious. ‎ ‎ ‎Sasa wengine wanasoma vitabu vingi, ‎Lakini maisha yao ni y...

‎Siri Ya Kusoma Vitabu Vingi Bila Kuvisahau.....

  ‎ ‎Kakaa/Dadaa Yangu... ‎ ‎Unasoma kitabu leo... kesho umesahau kila kitu. ‎Ushaona hiyo kitu? Inachosha. Inakatisha tamaa. ‎Unajikuta unasoma tu, lakini hamna unachobeba. ‎ ‎Kama umewahi kujisikia hivyo… karibu kwenye club yetu. ‎ ‎Lakini leo nataka nikuambie kitu cha maana sana. ‎Siri ambayo wengi hawajui. ‎Siri ya kusoma vitabu vingi bila kuvisahau. ‎Na kuvitumia kukuinua maishani. ‎ ‎ ‎Unasoma, unasahau. Unasoma, unasahau. ‎Kama vile ubongo wako unazima mara tu ukifunga kitabu. ‎Unajikuta unarejea kwenye maisha ya zamani. ‎ ‎Unasema “Aaah, kile kitabu kilikuwa kizuri sana…” ‎Lakini ukuliza ulijifunza nini? Unashindwa kusema. ‎ ‎Inaumiza. Sana. ‎Ni kama unakula chakula kizuri, lakini mwili wako haukipokei. ‎Hakuna nguvu. Hakuna mabadiliko. Hakuna matokeo. ‎ ‎Lakini tatizo si wewe. ‎Tatizo ni mbinu unayotumia. ‎Watu wengi husoma vitabu kama vile wanasoma gazeti. ‎ ‎Wanakimbia. Wanamaliza haraka. ‎Wanataka kumaliza kurasa nyingi bila kutafuna kilichoandikwa. ‎ ‎Halafu wanashanga...