‎🔥Siri Za Hadithi Zinazouza Kama Kichaa , Mfumo Wa The Hero’s Journey!🔥 ‎

Kakaa/Dadaa Yangu.... Wewe unajua kwanini hadithi zingine zinaburudisha mpaka unashindwa kutoka kwenye screen? ‎ ‎Unajua kwa nini mtu anakusimulia story mpaka unajikuta unaitikia, *Duh! Alafu ikawaje?* ‎ ‎Basi sikia hii... ‎ ‎Wauzaji wengi wanaandika hadithi ambazo hazigusi hisia. ‎Ni kama kuangalia movie ya kuchosha kwenye slow motion. ‎Wateja hawajali. Wanaskip. Wanapotea. ‎ ‎Lakini... ‎Kuna mfumo mmoja wa KISANII, wakisanii mbaya, ambao ukishaujua, utawakamata watu kama sumaku. ‎ ‎Unaitwa: Hero’s Journey. ‎ ‎Ni mfumo wa hadithi ya shujaa. ‎Yaani mtu wa kawaida, anakutana na changamoto, anapambana, anakata tamaa, anasimama tena, na mwisho anashinda. ‎ ‎Kama Simba kwenye Lion King. ‎Kama Neo kwenye Matrix. ‎Kama wewe kwenye maisha yako. ‎ ‎Sasa tatizo ni hili... ‎Watu wanajaribu kuuza bila kuleta safari ya kihisia. ‎Wanataka kuuza bidhaa kama vile ni maharage sokoni. ‎Wanakosa story. ‎Na bila story,hakuna connection. ‎ ‎Unasema bidhaa yako ni bora? So what? ‎Wateja wanataka kujihisi w...

‎Sanaa Ya Kuandika Kichwa Cha Habari Cha Kutosha Kuusimamisha MOYO Wa MTEJA


‎“Ukishika hii, unaweza kuuza barafu jangwa la Sahara”

‎Kakaa/Dadaa Yangu....


‎Unajua shida kubwa ya waandishi wengi wa matangazo?

‎Wanahangaika kuandika miandiko mizuri sana…

‎Lakini "kichwa cha habari chao ni cha kawaida sana".

‎Halafu wanashangaa kwa nini hakuna anaye-click.

‎Wanasema watu hawasomi.

‎Hapana.

‎Watu wanasoma

‎Wanasoma vichwa vya habari tu.

‎Kama kichwa hakishiki moyo…

‎Kama hakimshtui mteja…

‎Kama hakimfanyi asimame hata kama alikuwa anaenda chooni…

‎Hutauza kitu.

‎Unajua inakera kiasi gani kuandika post kali, halafu hakuna mtu ana-comment?

‎Halafu mtu mwingine anaandika tu:

‎"Siku zote pesa ziko mitaani."

‎Anapiga emoji 3 za moto.

‎Anapata likes 400.

‎Inakuchoma roho.

‎Unajisikia umechemka.

‎Unajiuliza, “Kwani shida iko wapi?”

‎Shida iko kwenye kichwa cha habari.

‎Hicho ndo mtego.

‎Na mtego ukikosa chambo, samaki hawezi kung’ang’ania.

‎Sasa sikia kaka/dada...

‎Kichwa cha habari siyo tu sentensi ya mwanzo.

‎Ni mlango.

‎Ni ngumi ya kwanza.

‎Ni busu la kwanza kwenye story.

‎Ni densi ya kwanza kwenye harusi.

‎Ukiboa hapo game imeisha.

‎Na hapa wengi wanaboi.

‎Wanatumia vichwa vilivyojaa maneno ya “kitaalamu”, “kawaida”, au “yasiyoamsha hisia”.

‎Hata chura wa bwawa hawezi kushtuka navyo.

‎Mfano mbaya:

‎“Jinsi ya kupata wateja wengi”

‎Huo ni mfu. Hauchochei hamu.

‎Sasa sikia kichwa kinachopiga kelele:

‎“Wateja Wako Hawakimbii Wewe Ndio Unawafukuza Bila Kujua

‎ (Soma Hii Kabla Hawajakutoka Kabisa!)”

‎Kichwa kama hicho?

‎Kinasimamisha moyo.

‎Suluhisho ni hili:

‎Andika kichwa kama mtu anayeandika SMS ya kuokoa mapenzi.

‎Kama mtu anayepiga kelele ya moto kwenye nyumba.

‎Kama mtu aliyepoteza wallet yenye mshahara wake wote.

‎Kichwa lazima kiwe na:

‎Shida.

‎Shtuko.

‎Siri.

‎Sababu ya mtu kusimama na kusoma.

‎Na unahitaji fomula kali.

‎Mojawapo ni hii hapa:

‎“(Ahadi Kubwa + Muda Mfupi + Hatari Ikikosewa)

‎Mfano:

‎“Jinsi Ya Kuandika Kichwa Kimoja Tu Kinachoweza Kukuletea Wateja 10 Bila Kulipia Tangazo Ukikosea Hii, Unaweza Kupoteza Fursa Za Mwaka Mzima!”

‎Ngoja nikupe story ya kweli.

‎Kuna jamaa mmoja aitwaye Kedi.

‎Anauza vifaa vya simu Instagram.

‎Alikuwa anapost picha tu.

‎Caption: “Zimefika mpya.”

‎Zero comments. Zero sales.

‎Nikampa kichwa hiki cha habari:

‎“Ukivaa Earbuds Mbovu, Unaweza Kukosana na Boss Bila Kujua, Angalia Hii Set Niliyokuwekea”

‎Broo!

‎Order 17 ndani ya siku 3.

‎DM zikawa nyingi kuliko likes.

‎Jamaa alinipigia usiku wa manane.

‎Akasema: “Nimeamini, kichwa cha habari ndio roho ya biashara.”

‎Sasa na wewe?

‎Usicheze na kichwa.

‎Ukikosa kichwa kizuri, maandiko yako hayana miguu.

‎Hayatembei.

‎Yanakufa.

‎Tumia muda mwingi kutunga kichwa—kuliko hata content.

‎Kwa sababu kichwa kikikamata moyo…

‎Hata maandiko yako ya kawaida yataonekana moto.

‎Na ukitaka nikusaidie kutunga vichwa vya habari vinavyosimamisha moyo kama betri mpya ya Tesla, niambie.

‎Mimi ni copywriter wako wa mtaa.

‎Na sipigi tu kelele nina rekodi ya kusababisha sales zisizotarajiwa.

‎Tuandike kichwa chako kesho?

‎Ama uendelee kupost “Zimefika mpya”?

‎Chaguo ni lako.

‎Kama Unataka Nikushike Mkono Andika "NATAKA KUWA COPYWRITER"

‎Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Ni Mimi Rafiki Yako Ninayekujali Sana.

‎Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection

Vitabu Gani Vilibadilisha Maisha Yangu?