Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Angalia Nguvu Ya Haya Maneno Matano (5) Yenye Kulevya – Maneno Yanayovutia Haraka Machoni.....



‎Rafiki Yangu Mpendwa,

‎Unajua shida kubwa ya wengi?

‎Wanaandika maneno ya kawaida mno.

‎Maneno yaliyokufa.

‎Hayana ladha. Hayagusi hisia.

‎Yanapitwa tu kama upepo.

‎Alafu wanashangaa...

‎Mbona hakuna anayesimama kusoma?

‎Mbona hakuna anayebonyeza?

‎Sasa leo nakuonyesha kitu kinono.

‎Maneno matano tu.

‎Lakini ni hatari.

‎Yana nguvu ya kuvuta macho ya mtu hata akiwa bize aje asome tu.

‎Hebu fikiria…

‎Umeweka post kali sana.

‎Unajua kabisa kuna madini.

‎Lakini hakuna mtu anaye-comment.

‎Hakuna likes. Hakuna saves.

‎Unakata tamaa.

‎Unaanza kufuta post zako.

‎Unaamini labda huwezi.

‎Unajua kwanini?

‎Ni kwa sababu kichwa cha habari yako kinapwaya.

‎Hakina mvuto.

‎Hakina “punch.”

‎Hakina kulevya.

‎Sikiliza kaka, dada...

‎Hili neno “karibu” ni zuri.

‎Lakini halina nguvu kama “karibu ujionee.”

‎Hili neno “soma” ni zuri.

‎Lakini halivutii kama “soma haraka kabla haijatolewa.”

‎Unashika pointi?

‎Lugha ya kuuza lazima iwe na mchele wa maneno ya moto.

‎Maneno ya kishindo.

‎Maneno yanayochoma kama pilipili nyekundu.

‎Kama unataka kuvuta macho ya mtazamaji…

‎Maneno haya ni silaha zako tano:

‎✅ “ANGALIA” – linaamsha macho. Linapiga stop.

‎✅ “SIRI” – linaficha lakini linavuta. Mtu anatamani kujua.

‎✅ “HARAKA” – linaongeza presha. Hali ya dharura.

‎✅ “SOMA HAPA” – linaelekeza. Linaita. Kama alarm.

‎✅ “USIPITE HAPA” – linakataza kwa njia inayovutia zaidi.

‎Haya ni maneno ya kutia chumvi kwenye kichwa cha habari.

‎Yakiwa kwenye sentensi, yanavuta macho kama sumaku.

‎Yanavuta vidole vya mtu vilivyo bize.

‎Anaswipe hadi asome.

‎Bado namkumbuka...

‎Dogo Wa Kinondoni Alivyogeuza Post Za Kupitwa Kuwa Za Kuchafua Notification

‎Kuna dogo anaitwa Jemo.

‎Anafanya biashara ya mashati ya kitenge Instagram.

‎Post zake zilikuwa kama hewa.

‎Anapost, lakini hakuna anayejali.

‎Nikamwambia:

‎“Bro, usianze na ‘karibu’ au ‘hello guys’… weka moto kichwani!”

‎Akaanza kutumia maneno haya matano.

‎Kichwa cha post kikawa kama:

‎“ANGALIA MASHATI HAYA YA KUPASUA MIOYO – USIPITE HAPA!”

‎Matokeo?

‎Within wiki moja…

‎Post moja ilifanya orders 74.

‎DM zikawa zinabana hadi akaweka WhatsApp link.

‎Leo hii, Jemo ni mmoja wa vijana wanaosumbua mtaani.

‎Kwa nini?

‎Kwa sababu aligundua nguvu ya maneno yenye kulevya.

‎Ujumbe Wa Mwisho Kwako...

‎Usiwe tu mtu wa kupost.

‎Kuwa msanii wa maneno.

‎Maneno matano tu…

‎Yanaweza kuwasimamisha watu kama muziki wa Diamond.

‎Anza kuandika kwa hisia.

‎Maneno ya moto.

‎Maneno ya kuvuta.

‎Maneno ya kulevya.

‎Ukitaka list ndefu ya maneno kama haya ya “kulevya macho”… niambie tu.

‎Nitakutumia kama zawadi ya copywriter. 😎🔥

‎Tuma meseji nataka kuwa "COPYWRITER"

‎Kwenda 0750376891.

‎Karibu.

‎Hii Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

‎Mkufunzi Ramadhan Amir

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Faida 7 Za Kipekee Za Kusoma VITABU Kila Siku Hata Kama Ni DAKIKA 10 TU!

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...