Machapisho

Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Hivi Ndivyo Nilivyopata Mteja Wangu Wa Kwanza Kwa Kalamu Tu!...

Picha
  ‎ ‎Kakaa/Dadaa yangu… ‎ ‎Hivii ushawahi kukaa na njaa hadi unaandika mawazo kwenye daftari badala ya kula? ‎ ‎Mimi nilishawahi. ‎ ‎Nilikuwa na ndoto ya kuwa copywriter. ‎Lakini sikujua nianzie wapi. ‎ ‎Zero network. ‎Zero pesa. ‎Na mbaya zaidi… ‎ ‎Watu hawakuamini kitu kama *kuandika matangazo* ni kazi. ‎ ‎Walinicheka. ‎Hawakuziamini ndoto zangu. ‎Wengine walinambia: ‎ ‎"We kaa tu uandike mashairi yako huko!" ‎ ‎Nilihisi kama naota ndoto ambayo haipo kwenye Google. ‎Lakini moyo haukukubali niachane nayo. ‎ ‎Ilikuwa Kama Ndoto Mbaya ‎ ‎Kila siku nilikuwa ninaamka asubuhi na kuchora matangazo kwenye daftari la zamani. ‎ ‎Hapo.... ‎ ‎Sina laptop. ‎Sina printer. ‎Nina tu kalamu ya cello na daftari la kasuku. ‎ ‎Nilijifunza kuandika matangazo yenye hisia. ‎Yale ya kumgusa mtu mpaka ashindwe kulala bila kukutafuta. ‎ ‎Lakini bado… ‎Hakuna mtu aliyekuwa anajua kuwa mimi ni copywriter. ‎ ‎Nilikuwa kivuli. ‎ ‎Hapo Ndo Nikapiga Stop ‎ ‎Nikajikumbusha ile kauli niliyoambiwaga na mento...

‎Kuna Maelfu Ya Vitabu… Lakini Hiki Ndicho Kimenibadilisha Zaidi!...

  ‎ Weh! ‎ ‎Kakaa/Dadaa... ‎ ‎Sina hata haja ya kuzunguka sana. ‎ ‎Kuna vitu unaweza kuvipitia kwenye maisha mpaka ukahisi kama unatembea juu ya miiba. ‎ ‎Unaamka kila siku asubuhi, unaenda kutafuta... lakini maisha hayabadiliki. ‎ ‎Unapiga kazi sana kama punda, lakini mkononi  huna hata senti 5. ‎ ‎Mpaka unajiuliza, “Hivi kweli kuna njia ya kutoka hapa nilipo?” ‎ ‎Na mimi nilikuwa hivyo. ‎ ‎Kichwa kimejaa mawazo. ‎Moyo umejaa hofu. ‎ ‎Pesa ni ndoto. ‎Na kila mtu anakushauri kusoma vitabu, eti vitakubadilisha. ‎ ‎Lakini ukiingia kwenye mtaa wa vitabu utakutana na maelfu ya vitabu. ‎Na kila kimoja kinajifanya kiko na suluhisho ya changamoto zako. ‎ ‎Ila unajua nini? ‎ ‎Vingi ni kama soda isiyo na gas. ‎Vina maneno mengi... ila havikusaidii chochote. ‎ ‎Ni kama kupewa ramani ya dunia nzima ukiwa umepotea mtaa wa pili. ‎ ‎Lakini hiki kitabu... ‎ ‎We acha tu niseme ukweli, ‎Hiki kitabu kilinitoa shimoni. ‎ ‎Ha...

‎Mbinu 3 Rahisi Zitakazokusaidia Na Kufanya Wateja Wakupende Bila Kujipendekeza…

 ‎ ‎Kakaa/Dadaa.... ‎ ‎Unajua shida kubwa ya wauzaji wengi ni nini? ‎ ‎Wanahangaika kuwafanya wateja wawapende… ‎ ‎Wanawafuata wateja kila kona… ‎ ‎Wanaomba omba mapenzi kama wahitaji… ‎ ‎Lakini bado… ‎Wateja hawawaoni! ‎Wateja hawawakumbuki! ‎Wateja hawasikii hata huruma! ‎ ‎Mbaya zaidi, kuna jamaa mwingine hajawahi hata kujitambulisha sana… ‎ ‎Lakini kila mteja anamuita, anamfuata, anamwamini! ‎ ‎Unajiuliza… *Kwa nini sio mimi?* ‎Kwa nini mimi ndo napigwa chenga kila siku? ‎ ‎Ngoja nikuambie kitu cha ukweli… ‎Wateja hawapendi mtu anayeomba sana. ‎ ‎Wanapenda mtu anayewaonyesha thamani… kimya kimya. ‎ ‎Na ndo maana leo nakupa hizi mbinu 3. ‎Mbinu za mtaa. ‎ ‎Rahisi sana… lakini zenye uzito wa almasi. ‎ ‎MBINU #1: Usijiuze, Jionyeshe ‎ ‎Acha kulalamika eti watu hawakunotisi… ‎Wewe jionyeshe tu kwa vitendo. ‎ ‎Jibu comment zao. ‎Watumie ujumbe unaosaidia bila kutegemea chochote. ‎Toa msaada mdogo mdogo kwenye status zako. ‎ ‎Wacha maneno mengi. ‎Tenda. ‎Waonyeshe kuwa upo… bila kuom...

Watu Wanaofeli Sio Kwa Kukosa Elimu… Wanakosa Hiki Kitu Kimoja Muhimu!

‎ ‎Kakaa/ Dadaa. ‎ ‎Kuna watu wengi sana wana akili. Wanasoma sana. Wana degree, wengine hadi masters. ‎ ‎Vitabu wanakula kama ugali. Lakini cha ajabu... maisha yao bado hayajanyooka. ‎ ‎Kama ni hela – hawana. ‎Kama ni mafanikio – hawana. ‎Kama ni amani – hawana. ‎ ‎Wewe pia unawajua. Au labda wewe mwenyewe ndio huyo. Unajiuliza, “Inawezekanaje? Na maarifa yote haya?” ‎ ‎ ‎Unaamka mapema. Unasoma vitabu vya watu waliowafikia kilele. Unaangalia YouTube, unahudhuria semina. Unajaza daftari kwa pointi motomoto. ‎ ‎Lakini bado huna kazi nzuri. ‎Bado hujaanza biashara yako. ‎Bado unahisi maisha yanakusukuma tu. ‎ ‎Ni kama vile unaenda shule kila siku, lakini hakuna mtihani unaopita. ‎ ‎Unajua nini kinauma zaidi? ‎Kumuona mtu ambaye hajui hata nusu ya unayojua , lakini anakupita kila kona! ‎ ‎Ana biashara, ana connections, ana mpango. Wewe una theory. Yeye ana matokeo. ‎ ‎Inaumiza. ‎ ‎ ‎Maarifa ni muhimu. Usivichukie vitabu. Lakini… ‎Maarifa peke yake HAYATOSHI. ‎ ‎Kusoma bila kuchukua hat...

Jinsi Ya Kujitambulisha Kama Mtaalamu Mtandaoni Bila Kuonekana Kama Unajigamba.

 ‎ ‎‎Kakaa/Dadaa... ‎ ‎Unajua shida ni nini? ‎Watu wanajituma sana mtandaoni. ‎Wanapiga picha za ofisini. ‎Wanaandika "DM me for business". ‎Wengine mpaka wanajiita Expert. ‎ ‎Lakini bado… hakuna anaowauliza kitu. ‎Hakuna anawachukulia serious. ‎ ‎Unapiga kelele, lakini hakuna anayesikia. ‎ ‎Inauma, eeh? ‎Unatoa elimu bure. ‎Unajituma kila siku. ‎Lakini kila post yako inapata like nne. ‎Na zote ni kutoka kwa ndugu zako. ‎ ‎Watu hawakuoni kama mtaalamu. ‎Wanakuchukulia kawaida. ‎Na mbaya zaidi – unachoka. ‎Unaanza kujiuliza, "Labda hii sio njia yangu..." ‎ ‎Pole sana kaka/dada. ‎Tatizo sio wewe. ‎Tatizo ni mfumo wako wa kujitangaza. ‎ ‎Kuna kitu watu wengi hawajui. ‎Kujitambulisha kama mtaalamu sio kusema "Mimi ni mtaalamu." ‎Wala sio kuweka picha na caption ndefu ya kujisifu. ‎ ‎Hiyo ni sauti ya kelele. ‎Na watu wa mtandaoni wanachoka kelele. ‎Wanataka kitu kinachogusa. ‎Kinachofaa. ‎Kinachosaidia. ‎ ‎Ukijitangaza vibaya watu wanakuchoka kabla hata hawajak...

Kwa Nini Watu Wanakosa Pesa Ingawa Wanajituma?

‎Kakaa/Dadaa… ‎ ‎Umeshawahi kulala ukiwa umechoka sana, ‎ ‎Lakini bado huna hata shilingi mfukoni? ‎ ‎Umeamka mapema, ‎ ‎Ukapambana jua hadi linazama, ‎ ‎Ukavumilia kelele za mabosi, ‎Ukavumilia njaa kwa matumaini. ‎ ‎Lakini mwisho wa mwezi, ‎unahesabu senti. ‎ ‎Unaambiwa: *Jitume zaidi.* ‎Lakini unaumia moyoni, ‎kwa sababu umeshajituma mpaka unaungua ndani. ‎ ‎Kama hii ni hali yako, ‎najua uchungu unaoupitia. ‎ ‎Ni kama mbio zisizo na mwisho. ‎ ‎Unakimbia, lakini huoni mbele. ‎ ‎Unapiga hatua, lakini ni kama umerudi nyuma. ‎ ‎Wengine wanakucheka. ‎Wanasema huna akili ya pesa. ‎Lakini hawajui mateso yako. ‎ ‎Sasa sikiliza kwa makini... ‎ ‎Kazi ngumu pekee haitoshi. ‎Inauma kusema, lakini ni kweli. ‎ ‎Watu wengi wanaishia kuishi maisha ya mateso, ‎si kwa sababu hawajitumi, ‎bali kwa sababu hawajui cha kufanya na wanachopata. ‎ ‎Wanatumia kila walichonacho. ‎Hakuna mpango. ‎Hakuna akiba. ‎Hakuna uwekezaji. ‎Hakuna ndoto inayoelekea kutimia. ‎ ‎Na hapo ndipo ndoto nyingi hufia. ‎Ndipo ndo...

‎COPYWRITING: Sanaa Ya Kuandika Maneno Yanayouza.

  ‎  Ndiyo Leo. ‎ ‎Kakaa/Dadaa... ‎ ‎Kuna biashara kibao zinafungwa. ‎ ‎Maduka yamejaa bidhaa. ‎ ‎Lakini wanunuzi hakuna. ‎ ‎Wako tu online wakiskrol skrini hadi macho yaume. ‎ ‎Unashangaa mbona hawaombi bei? ‎ ‎Mbona hawaulizi details? ‎ ‎Mbona hawaingii DM? ‎ ‎Tatizo si bidhaa zako. ‎ ‎Tatizo si bei yako. ‎ ‎Tatizo ni maneno yako. ‎ ‎Maneno yako hayaendi na mwendo wa wateja wa sasa. ‎ ‎Hayagusi. Hayachomi. Hayatishi. Hayavutii. ‎ ‎Unahitaji Copywriting. ‎ ‎Maneno yanayouza. ‎ ‎Maneno yanayopenya hadi kwenye roho ya mteja. ‎ ‎Sasa ngoja nikuambie ukweli mchungu... ‎Kama bado unaandika post za “karibu sana” ‎ ‎Au *nauza viatu vizuri bei nafuu* ‎ ‎Wewe ni kama mtu anayeimba kwenye jumba tupu. ‎ ‎Utaimba hadi koo likauke… lakini hakuna anayesikia. ‎ ‎Wenzako wanapost mara moja, wanapata order 30. ‎ ‎Wewe unashusha bei hadi unauza kwa hasara. ‎ ‎Na bado kimya. ‎ ‎Bado hakuna anayebonyeza link yako. ‎ ‎Hata likes hazifiki kumi. ‎...