Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

‎Hivi Ndivyo Nilivyopata Mteja Wangu Wa Kwanza Kwa Kalamu Tu!...

 


‎Kakaa/Dadaa yangu…

‎Hivii ushawahi kukaa na njaa hadi unaandika mawazo kwenye daftari badala ya kula?

‎Mimi nilishawahi.

‎Nilikuwa na ndoto ya kuwa copywriter.

‎Lakini sikujua nianzie wapi.

‎Zero network.

‎Zero pesa.

‎Na mbaya zaidi…

‎Watu hawakuamini kitu kama *kuandika matangazo* ni kazi.

‎Walinicheka.

‎Hawakuziamini ndoto zangu.

‎Wengine walinambia:

‎"We kaa tu uandike mashairi yako huko!"

‎Nilihisi kama naota ndoto ambayo haipo kwenye Google.

‎Lakini moyo haukukubali niachane nayo.

‎Ilikuwa Kama Ndoto Mbaya

‎Kila siku nilikuwa ninaamka asubuhi na kuchora matangazo kwenye daftari la zamani.

‎Hapo....

‎Sina laptop.

‎Sina printer.

‎Nina tu kalamu ya cello na daftari la kasuku.

‎Nilijifunza kuandika matangazo yenye hisia.

‎Yale ya kumgusa mtu mpaka ashindwe kulala bila kukutafuta.

‎Lakini bado…

‎Hakuna mtu aliyekuwa anajua kuwa mimi ni copywriter.

‎Nilikuwa kivuli.

‎Hapo Ndo Nikapiga Stop

‎Nikajikumbusha ile kauli niliyoambiwaga na mentor wangu:

‎*Bro, kama huwezi kuingia kwa milango ya mbele, pita dirishani.*

‎Nikaanza kuandika tangazo kali kama sample.

‎Kalamu tu na karatasi.

‎Nikakaa chini, nikamtengenezea tangazo jamaa mmoja niliyemfahamu kwenye Instagram.

‎Anauza viatu.

‎Sikutuma DM.

‎Sikutuma email.

‎Nilipiga print hiyo kazi kwa shilingi 50 TU stationary.

‎Nikafungasha vizuri.

‎Nikaenda kwao kama mteja wa kawaida.

‎Baada ya kuongea kidogo nikamwambia:

‎"Bro, kuna kitu nimeandika… Naamini kitakusaidia kuuza viatu vyako faster."

‎Alisoma.

‎Akatulia.

‎Akatabasamu.

‎Akanitazama machoni.

‎Akasema:

‎"Bana, hii kitu ni moto wa kuotea mbali!"

‎Ndiyo hivyo…

‎Mteja wa kwanza nilivyompata.

‎Na aliingia kwa sababu ya kalamu tu.

‎Ndio Nikajifunza Siri Hii

‎Watu hawataamini unachoweza…

‎Mpaka uwaonyeshe kwa vitendo.

‎Sio kuomba.

‎Sio kusubiri.

‎Onyesha tu kazi yako hata kama ni bure mara ya kwanza.

‎Na kama unaamini kuwa huwezi kuanza sababu hauna tools…

‎Ngoja nikwambie ukweli mchungu:

‎Huna njaa ya kweli.

‎Mwenye njaa ya kweli, hata kalamu inamtosha kabisa.

‎Leo hii…

‎Ninavyoandika hivi, nina wateja kutoka ndani na nje ya nchi.

‎Lakini nilianza na karatasi na kalamu tu.

‎Hakuna shortcut.

‎Ni damu, jasho na mistari ya kugusa moyo.

‎Kama Wewe Ni Kama Mimi...

‎Kama unahisi upo peke yako.

‎Kama unaandika lakini hakuna anayekuamini.

‎Kama watu wanakudharau kwa vile kazi yako *haionekani*…

‎Jua kwamba kuna mtu mmoja tu unayemhitaji akuamini.

‎Na huyo mtu ni wewe mwenyewe.

‎Tulia.

‎Andika.

‎Sambaza kazi yako.

‎Usiombe nafasi.

‎Itengeneze.

‎Kalamu ndiyo silaha yangu.

‎Na kama mimi niliweza,

‎basi hata wewe unaweza.

‎Kama unataka mwongozo kamili ulionifikisha hapa.

‎Bonyeza Hapa 👇 

‎*https://wa.link/pz47ru*

‎Karibu

‎0750376891.

‎Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection