Siri Za Hadithi Za Mauzo...

 *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Rafiki Yangu, Wauzaji wengi wanahangaika kuandika matangazo yanayouza. Wanaandika, lakini hakuna anayeona, hakuna anayeuliza, hakuna anaye nunua. Ni maumivu makali kuona mtu mwingine anauza bidhaa kama yako, Lakini wewe unabaki unalalamika *soko ni gumu.* Kitabu *Siri Za Hadithi Za Mauzo* Kinakuonyesha namna ya kuandika hadithi zinazogusa mioyo, zinazoeleza, zinasisimua, na hatimaye zinauza. Utajifunza kuandika maandiko yanayovutia macho, yanayobeba hisia, na yanayobadilisha wasomaji kuwa wanunuzi. Pata nakala yako leo. Kwa kuwasiliana na 0755376891. PS; Anza kuandika hadithi zinazouza badala ya maneno yasiyoleta matokeo.

Kwa Nini Watu Wanakosa Pesa Ingawa Wanajituma?



‎Kakaa/Dadaa…
‎Umeshawahi kulala ukiwa umechoka sana,
‎Lakini bado huna hata shilingi mfukoni?
‎Umeamka mapema,
‎Ukapambana jua hadi linazama,
‎Ukavumilia kelele za mabosi,
‎Ukavumilia njaa kwa matumaini.
‎Lakini mwisho wa mwezi,
‎unahesabu senti.
‎Unaambiwa: *Jitume zaidi.*
‎Lakini unaumia moyoni,
‎kwa sababu umeshajituma mpaka unaungua ndani.
‎Kama hii ni hali yako,
‎najua uchungu unaoupitia.
‎Ni kama mbio zisizo na mwisho.
‎Unakimbia, lakini huoni mbele.
‎Unapiga hatua, lakini ni kama umerudi nyuma.
‎Wengine wanakucheka.
‎Wanasema huna akili ya pesa.
‎Lakini hawajui mateso yako.
‎Sasa sikiliza kwa makini...
‎Kazi ngumu pekee haitoshi.
‎Inauma kusema, lakini ni kweli.
‎Watu wengi wanaishia kuishi maisha ya mateso,
‎si kwa sababu hawajitumi,
‎bali kwa sababu hawajui cha kufanya na wanachopata.
‎Wanatumia kila walichonacho.
‎Hakuna mpango.
‎Hakuna akiba.
‎Hakuna uwekezaji.
‎Hakuna ndoto inayoelekea kutimia.
‎Na hapo ndipo ndoto nyingi hufia.
‎Ndipo ndoto nyingi hulia kwa ukimya.
‎Lakini bado kuna tumaini...
‎Siku utakapoamua kufikiri tofauti kuhusu pesa,
‎Ndipo utakapogeuza mwelekeo wa maisha yako.
‎Pesa si adui.
‎Pesa si ya kuikimbiza bila kuelewa.
‎Pesa ni mti unaoota pale unapopanda mbegu sahihi.
‎Anza kuipangilia.
‎Anza kuwekeza.
‎Anza kuiona kama njia ya kutimiza ndoto zako.
‎Nakupa mfano...
‎Kuna kijana mmoja, Ali.
‎Kila siku alikuwa kwenye jua, kwenye vumbi, kwenye jasho.
‎Lakini maisha yake yalikuwa yale yale. 
‎Migongoni mwa daladala,
‎maskani ya huzuni.
‎Mpaka siku rafiki yake alivyomfundisha kitu kimoja,
‎Kuiheshimu pesa.
‎Kuipangilia.
‎Kuwekeza hata kidogo.
‎Ali akachukua hatua ndogo.
‎Na hatua hiyo iligeuka kuwa maisha mapya.
‎Miaka michache baadaye akamiliki nyumba,
‎Ana biashara yake mwenyewe.
‎Si kwa sababu alikuwa na bahati.
‎Ni kwa sababu alijifunza kutumia pesa kwa akili.
‎Na wewe pia unaweza.
‎Usikubali maisha yako yawe hadithi ya maumivu yasiyoisha.
‎Chukua hatua.
‎Jifunze sasa.
‎Badilisha maisha yako.
‎Piga Simu: 0750376891
‎Nitakusaidia.
‎Tutapambana pamoja.
‎Mpaka uzishike ndoto zako mkononi.
‎Mkufunzi Ramadhan Amir
‎0750376891

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

‎Mbinu 7 Za Kukumbuka Unachosoma Katika Vitabu Bila KUSAHAU TENA... ‎

‎Jinsi Ya Kutumia Vitabu Kujenga Maisha Na Biashara Bila Mtaji Mkubwa...

‎Hatua 7 Rahisi Za Kuanzisha Ndoto Yako Bila Mtaji Mkubwa- Hata Kama Huna Connection