COPYWRITING: Sanaa Ya Kuandika Maneno Yanayouza.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Ndiyo Leo.
Kakaa/Dadaa...
Kuna biashara kibao zinafungwa.
Maduka yamejaa bidhaa.
Lakini wanunuzi hakuna.
Wako tu online wakiskrol skrini hadi macho yaume.
Unashangaa mbona hawaombi bei?
Mbona hawaulizi details?
Mbona hawaingii DM?
Tatizo si bidhaa zako.
Tatizo si bei yako.
Tatizo ni maneno yako.
Maneno yako hayaendi na mwendo wa wateja wa sasa.
Hayagusi. Hayachomi. Hayatishi. Hayavutii.
Unahitaji Copywriting.
Maneno yanayouza.
Maneno yanayopenya hadi kwenye roho ya mteja.
Sasa ngoja nikuambie ukweli mchungu...
Kama bado unaandika post za “karibu sana”
Au *nauza viatu vizuri bei nafuu*
Wewe ni kama mtu anayeimba kwenye jumba tupu.
Utaimba hadi koo likauke… lakini hakuna anayesikia.
Wenzako wanapost mara moja, wanapata order 30.
Wewe unashusha bei hadi unauza kwa hasara.
Na bado kimya.
Bado hakuna anayebonyeza link yako.
Hata likes hazifiki kumi.
Si kwasababu bidhaa zako hazivutii.
Ni kwasababu maneno yako hayawezi kuuza hata toothpick.
Copywriting ni zaidi ya kuandika tu.
Ni kuandika kwa makusudi.
Kila neno lina kazi.
Kila sentensi ni mshale unaoenda moja kwa moja kwenye moyo wa mteja.
Na sio lazima uwe na degree.
Sio lazima uwe na Kiswahili fasaha.
Sio lazima uwe na kompyuta.
Unachohitaji ni kujua namna ya kuongea na mteja kwa lugha anayopenda.
Kwa lugha inayoamsha tamaa zake.
Kwa lugha inayomgusa hadi ashindwe kupumua bila kubonyeza Nunua Sasa.
Acha kabisa ile dhana ya “Nikisema ukweli bidhaa yangu itajiuza yenyewe.”
Hakuna kitu kama hicho.
Bidhaa haijiuzi.
Copywriting ndiyo huuza bidhaa.
Suluhisho ni rahisi.
Jifunze Copywriting.
Jifunze kuandika maneno yanayovuta macho.
Maneno yanayoamsha hisia.
Maneno yanayopenya hadi kwenye mfuko wa mteja.
Ukiweza kuandika post moja yenye nguvu…
Unaweza kuuza bidhaa hata ukiwa na followers mia tu.
Na si kuandika ovyo…
Ni kutumia fomula.
Ni kutumia psychology.
Ni kuelewa uchungu wa mteja…
Halafu unamwonyesha kwamba bidhaa yako ndiyo dawa ya maumivu yake.
Hapo nyuma...
Nilikuwa nafanya kazi ya kawaida tu.
Naandika caption za kawaida kwenye page yangu.
Posti zilikuwa zinaishia kwa likes mbili na comment moja ya binamu.
Siku moja nikajifunza Copywriting.
Nikaanza kuandika kwa kutumia hisia.
Nikaanza kutumia maneno yanayouza.
Nikaanza kuelewa namna ya kugusa maumivu ya wateja.
Posti yangu ya kwanza ya "Copywriting" ilileta order 12 ndani ya siku moja.
Na hapo nilijua:
Maneno yana nguvu kuliko picha.
Leo hii naandika post moja,
Napata wateja wa wiki nzima.
Nimeandika matangazo kwa watu walikua hawauzi kabisa, sasa wanachoka kupeleka mzigo kila siku.
Copywriting imenitoa mbali.
Na inaweza kukutoa pia.
Mwisho kabisa…
Usiseme nitajifunza kesho.
Kesho haitambui njaa yako ya leo.
Ndiyo Leo.
Chukua hatua.
Jifunze Sanaa ya Kuandika Maneno Yanayouza.
Kama umeisoma hadi hapa una kiu.
Kama una kiu utainywa.
Na maji yako ni COPYWRITING.
Kujifunza zaidi kuhusu ujuzi wa copywriting,
Tuma ujumbe *NATAKA COPYWRITING*
Kwenda 0750376891.
Karibu.
Mkufunzi Ramadhan Amir
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni