Jinsi Ya Kujitambulisha Kama Mtaalamu Mtandaoni Bila Kuonekana Kama Unajigamba.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Kakaa/Dadaa...
Unajua shida ni nini?
Watu wanajituma sana mtandaoni.
Wanapiga picha za ofisini.
Wanaandika "DM me for business".
Wengine mpaka wanajiita Expert.
Lakini bado… hakuna anaowauliza kitu.
Hakuna anawachukulia serious.
Unapiga kelele, lakini hakuna anayesikia.
Inauma, eeh?
Unatoa elimu bure.
Unajituma kila siku.
Lakini kila post yako inapata like nne.
Na zote ni kutoka kwa ndugu zako.
Watu hawakuoni kama mtaalamu.
Wanakuchukulia kawaida.
Na mbaya zaidi – unachoka.
Unaanza kujiuliza, "Labda hii sio njia yangu..."
Pole sana kaka/dada.
Tatizo sio wewe.
Tatizo ni mfumo wako wa kujitangaza.
Kuna kitu watu wengi hawajui.
Kujitambulisha kama mtaalamu sio kusema "Mimi ni mtaalamu."
Wala sio kuweka picha na caption ndefu ya kujisifu.
Hiyo ni sauti ya kelele.
Na watu wa mtandaoni wanachoka kelele.
Wanataka kitu kinachogusa.
Kinachofaa.
Kinachosaidia.
Ukijitangaza vibaya watu wanakuchoka kabla hata hawajakujua.
Sasa hivi, unachotakiwa kufanya ni hivi:
Jionyeshe kwa matokeo, si maneno.
Badala ya kusema “Mimi ni copywriter,”
Onyesha jinsi ulivyomsaidia mteja akuze mauzo.
Badala ya kusema “Mimi ni coach,”
Eleza story ya mteja aliyebadilika kupitia usaidizi wako.
Watu wanaamini matokeo.
Watu wanataka proof.
Watu hawataki kelele – wanataka msaada.
Jenga imani kimya kimya.
Toa elimu inayobeba uzoefu.
Toa thamani kabla ya kuomba hela.
Ukifanya hivi watu wataanza kukuona.
Mi mwenyewe nilikuwa naandika post ndefu sana.
Nilijipa majina ya ajabu: “Sales Wizard”, “Brand Genius” na mengine mengi.
Lakini hakuna aliyejibu inbox.
Mpaka nilipoamua kubadilika.
Siku moja nikaandika tu:
“Leo client wangu kaongeza mauzo kutoka elfu 40 mpaka laki 2 ndani ya siku 6. Nimefurahi kwake kuliko kwangu.”
Comment 28.
Inbox 9.
Na niliuza huduma zangu bila kupiga kelele.
Siri ni moja tu kaka:
Ongea kwa matokeo, si kwa maneno.
Watu hawataki kujua jina lako wanataka kuona kazi yako.
Chukua hili somo.
Anza leo.
Usiwe mpiga kelele mwingine mtandaoni.
Jionyeshe kimya kimya,
Utaonekana kwa kishindo.
Kujifunza ujuzi wa copywriting kwa kiswahili rahisi,
Au kama unataka kuandika matangazo yako mwenyewe,
Piga simu namba 0750376891.
Karibu.
Mkufunzi Ramadhan Amir.
Jisajili Hapa Upate Vitabu 10- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni