Watu Wanaofeli Sio Kwa Kukosa Elimu… Wanakosa Hiki Kitu Kimoja Muhimu!
Kakaa/ Dadaa.
Kuna watu wengi sana wana akili. Wanasoma sana. Wana degree, wengine hadi masters.
Vitabu wanakula kama ugali. Lakini cha ajabu... maisha yao bado hayajanyooka.
Kama ni hela – hawana.
Kama ni mafanikio – hawana.
Kama ni amani – hawana.
Wewe pia unawajua. Au labda wewe mwenyewe ndio huyo. Unajiuliza, “Inawezekanaje? Na maarifa yote haya?”
Unaamka mapema. Unasoma vitabu vya watu waliowafikia kilele. Unaangalia YouTube, unahudhuria semina. Unajaza daftari kwa pointi motomoto.
Lakini bado huna kazi nzuri.
Bado hujaanza biashara yako.
Bado unahisi maisha yanakusukuma tu.
Ni kama vile unaenda shule kila siku, lakini hakuna mtihani unaopita.
Unajua nini kinauma zaidi?
Kumuona mtu ambaye hajui hata nusu ya unayojua , lakini anakupita kila kona!
Ana biashara, ana connections, ana mpango. Wewe una theory. Yeye ana matokeo.
Inaumiza.
Maarifa ni muhimu. Usivichukie vitabu. Lakini…
Maarifa peke yake HAYATOSHI.
Kusoma bila kuchukua hatua ni kama kupika bila kula. Unajichosha bure.
Kusoma bila msaada wa mentor ni kama kuendesha gari bila ramani.
Unaenda tu… lakini hujui kama unakaribia au unazunguka hapo hapo tu.
Na maarifa mengi yanakulisha uongo. Yanakuambia "kuwa mvumilivu," "siku yako inakuja," "soma sana halafu mambo yatakaa sawa."
Hapana. Dunia ya leo inataka mtu anayejua na ANAYECHUKUA HATUA.
Unahitaji zaidi ya maarifa.
Unahitaji MPANGO – wa vitendo.
Unahitaji MENTOR – akuonyeshe njia, akuambie ukweli, akupush unapozubaa.
Unahitaji NETWORK – watu wanaoamini katika ndoto zako, si wakukebehi.
Unahitaji MAZINGIRA MAZURI , sio kila mtu anakufaa kwenye safari yako.
Na zaidi ya yote...
Unahitaji UTENDAJI.
Maarifa yako ni bure kama huwezi kuamka na kuyatumia.
Kuna kijana mmoja nilimfundisha copywriting. Alikuwa na degree ya biashara, lakini alikuwa hana kazi. Alikuwa anasoma kila siku.
... lakini hana hela hata ya bando.
Nikamuambia: “Bwana mdogo, acha kusoma kila siku.
Chukua hiki unachojua, andika tangazo moja tu. Moja.”
Alikataa mwanzo.
Alisema bado hajajua vya kutosha.
Nikambembeleza. Nikamwonyesha jinsi.
Leo hii, anaandika matangazo kwa kampuni tatu kubwa.
Na kipato chake… ni zaidi ya mshahara wa mtu mwenye digrii mbili.
Sio maarifa yaliyombadilisha. Ni hatua.
Maarifa bila hatua ni mzigo.
Lakini maarifa yaliyofungwa na hatua, maamuzi, na mentorship, hayo ndio yana nguvu.
Unataka kubadilisha maisha yako?
Usisome tu.
Tafuta mwongozo.
Tafuta hatua.
Tafuta msaada.
Maarifa yanakuandaa...
Lakini utendaji ndio unaokupa ushindi.
Kama unataka mentor wa kukupa mwongozo na kukushika Mkono,
Tuwasiliane Kwa Simu NAMBA 0750376891.
Tuma Ujumbe *NATAKA UWE KOCHA WANGU*
Kwenda 0750376891.
Karibu.
Mkufunzi Ramadhan Amir,
Mwandishi Wa Vitabu|Nguvu Ya Vitabu||Skript Za Mauzo|
Maoni
Chapisha Maoni